Sunday, May 31, 2009

MIsri, Sudan walie tu

Wakati nchi za Misri na Sudan zikiendelea kulilia sheria ya mkoloni inayoziruhusu kuwa na haki pekee ya kutumia maji ya Ziwa Victoria, Tanzania jana ilizindua mradi wa maji wa Sh244 bilioni ($200m) utakaosaidia wananchi wa mikoa ya Mwanza na Shinyanaga.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Martha Philipo kutoka katika kijiji cha Iselamagazi, Shinyanga, mara baada ya kuteka maji na kumtwisha ndoo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha kuchotea maji iliyofanyika kijijini hapo jana jioni. Kituo hicho ni moja kati ya vingi vya kuchotea maji vilivyo katika mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga. Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya. (Ikulu)

No comments:

Post a Comment