Tuesday, March 10, 2009

Maulid Njema

Salamu za Mdau...

Waislamu wapinga ubaguzi wa ajira za Bunge

Hivi karibuni nilipokea waraka toka kwa Taasisi moja ya Kiislamu nchini inayoelezea ubaguzi na upendeleo wa ajira katika nafasi zilizotolewa hivi karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa waraka huo,Bunge kupitia Gazeti la Mwananchi la Desemba 12 mwaka jana,lilitangaza nafasi za Hansard Reporter,Assistant Clerk na Computer Systems Analyst.

Hoja ni kuwa,waliyoomba nafasi hizo ni wengi,lakini kinachozungumzwa na kulalamikiwa ni kuwa waombaji wengi wametoka Chuo kimoja cha St. Agustine kulikoni? Waraka huu umesambazwa, nami nimebahatika kupata nakala. Interview ya nafasi hizo, imepangwa kufanyika Machi 10 mwaka huu. Nanyi mnaweza kufuatilia na kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli.
Ahsante.

No comments:

Post a Comment