Friday, December 28, 2007

UCHAGUZI KENYA: Makamu wa Rais Ashindwa Ubunge

Makamu wa Rais wa Kenya, Moody Awori, na Mawaziri wengine 18 wameshindwa Ubunge. Hilo ni pigo la kwanza kwa serikali ya Kibaki. Hata kama atashinda urais, mambo yatamwendea kombo kuongoza serikali yake kwa kuwa hatakuwa na wabunge wa kutosha kutoa maamuzi.
Katika matokeo ya awali ODM ya Rail Odinga imejipatia viti vya ubunge 77, wakati PNU ilikuwa imejipatia kura 19, huku ODM-Kenya viti 7, KANU 3, Safina 3, Narc 2, Ford Kenya 2.
Hadi kufikia jana jioni jumla ya mawaziri 18, wengi wao wakiwa marafiki wa karibu wa rais Kibaki wamepoteza viti vyao.
Baadhi ya mawaziri hao ni Moody Awori ambaye alikuwa Makamu wa Rais na Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Mambo ya Nje, Raphael Tuju, Waziri wa Biashara na Viwanda Mukhisa Kituyi na Waziri wa Mazingira ambaye pia alikuwa msaidizi wa Rais Kibaki wakati alipokuwa kiongozi wa upinzani nchini humo David Mwiraria.
Wengine waliopoteza viti vya ubunge na wizara zao kwenye mabano ni Mutahi Kagwe (Habari na Mawasiliano), Newton Kulundu (Kazi), Paul Sang (Afya), Simeon Nyachae (Barabara), Musikari Kombo (Serikali za Mitaa), Njenga Karume (Ulinzi).

No comments:

Post a Comment