Wednesday, October 24, 2007

Ijue ANGUKA

Anguka ni neo la Kiswahili linalomaanisha enda chini, kwa ghafla, poromoka, bugwa (kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili Sanifu). Lakini anguka ninayotaka kueleza hapa leo ni ile ya kifupi cha kaulimbiu ya Rais Jakaya Kikwete iliyomuingiza madarakani kwa kishindo cha asilimia zaidi ya 80. Yaani, Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya kifupi, ANGUKA. Wakati wahusika wakiinadi kaulimbiu hii, hawakujua kuwa kifupi chake kitakuja kufanana na hali halisi ndani ya miaka miwili ya utawala...Kwani wengine wanasema, Kasi mpya wanayoiona ni ya kurudi nyuma.

No comments:

Post a Comment