Wednesday, July 25, 2007

Nani kaiona ndege ya JK ikipaa?

Baada ya kushika madaraka ya juu kabisa nchini, Rais JK alisema ndege ya uchumi ya aliyokuwa ameiwasha Mtangulizi wake, Mkapa, ameikuta kwenye runway ikitaka kuruka. Alifafanua zaidi kuwa kazi yake kubwa itakuwa ni kuirusha ili Tanzania ipae. Yeye hajatamka lolote hadi sasa, lakini 'mbia wake' Ed ameshatamka kuwa ndege hiyo imeshapaa muda mrefu. Mimi sijaiona, ila nadhani imerudi kuegeshwa au haikuwa na mafuta. Wewe je, umeiona? Mwanakijiji mmoja naye amesema hajaiona, lakini ofisi ya Ed imejibu kwa besi kuwa ndege hiyo imesharuka muda mrefu...kalagabao wasioiona labda wana dhambi au hawatumii rada ya mtumba iliyonunuliwa kwa bei mbaya-RSM-

3 comments:

Simon Kitururu said...

Nafikiri Ofisi ya Ed walichanganya swali. Nafikiri walifikiri kuwa wanaulizwa kuhusu ungo. Ungo inawezekana umepaa na safari zake usiku watu wakiwa wamelala.

Ansbert Ngurumo said...

Mimi nimeiona. Inaitwa inflation. Wewe bado hujaiona?

Simon Kitururu said...

Samahani, natoka nje ya somo!

Njoo tumalizie kujadili kipengele, ili tuende kwenye hatua nyingine ya kuboresha wanajumuiya wa jumuiya ya Watanzania wanao tembelea au wanao blogi.

Tembelea hapa : http://blogutanzania.blogspot.com/
ilia tumalize kujazia dondoo ili tu anze na kipengele kingine.
Idumu JUMUWATA!

Post a Comment