Tuesday, July 17, 2007

Swali la leo Julai 17

Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Zakia Meghji imetangaza kuwa wafanyabiashara wa mafuta ya petroli na dizeli hawaruhusiwi kupandisha bei ya mafuta hayo zaidi ya Sh1,400 kwa kuwa mafuta waliyo nayo sasa hajaanza kutozwa kodi mpya. Meghji hakuishia hapo, aliziagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (UWURA). Lakini hakuna mabadiliko na wafanyabiashara 'wameweka pamba masikioni'. Je, wafanyabiashara wana nguvu kuliko serikali, au serikali ilitambua kuwa hilo haliwezekani, bali ilitaka wananchi waone wanatetewa?

No comments:

Post a Comment