Friday, May 19, 2006

Mtoto Aliyetekwa Nyara Dar Apatikana

Mzazi utamuelewa. Jeff Msangi aliandika habari hii kwa uchungu sana.
Hata waliochangia hoja hiyo, niiwemo mimi, waliijadili kwa uchungu
mkubwa. Kwa uchungu huo, Jeff aliamua pia kunipigia simu ili upata
maelezo ya kina kuhusu mtoto huyu wa miaka mitatu (3) Humud Aboubakar, aliyekuwa ametekwa nyara na maharamia wa Dar es salaam waliokuwa wanataka sh 5 m ili waweze kumuachia.

Habari Njema:
Gazeti la ThisDay liliripoti kurejeshwa kwa mtoto huyo, na kutelekezwa katika baa ya Excutive ya Mgomeni Kagera jijini Dar es Salaam. Inavyoonekana, hata hizo pesa sh 5 m walizotaka watekaji hawakuzipata na kila dalili zinaonyesha kuwa watu sita waliokamatwa kwa mahojiano wanaweza kuwa hawasiani na tukio hilo, kwani mhusika haswa alishafanikiwa kumtelekeza mtoto huyo bila kushtukiwa. ThisDay linapatikana hapa

7 comments:

Jeff Msangi said...

Miruko,
Ahsante sana kwa habari hizi njema.Kidogo nimepumua.Lakini maswali kuhusu mchango wa jeshi letu la polisi yanabakia pale pale kwa sababu inaonekana jamaa wamemrudisha kwa huruma zao tu.Miruko kama unaweza tafadhali nitafutie nambari za simu za hiyo familia.

zemarcopolo said...

jeff nimeguswa na jinsi ulivyoguswa na hili swala.pole ndugu yangu.jeshi letu la polisi lina matatizo yake,ila ukweli unabaki palepale UMASKINI.katika nchi ambayo hata mitaa haijulikani ni vigumu sana kwa jeshi maskini kama letu kufanya kazi kwa kiwango ridhisho.mimi naiona hii kama vicious circle!!!

ndesanjo said...

Siku zinavyokwenda mbinu za kujipatia fedha kwa haraka zinaongezeka na kubadilika. Hatua hii ya kuanza kuteka watoto inatisha na kusikitisha. Jeff na wewe mmetupa vyema habari hii inayotia huzuni sana. Huwezi kuamini kuwa nchi inayozungumziwa ni Tanzania.

Boniphace Makene said...

Nilishukuru sana baada ya kusoma habari ya kupatikana mtoto huyu. Niwashukuru nanyi pia kwa kuifunua habari hii na kweli mmeonyesha namna mnavyowajali watu wadogo. Mungu awabariki

Anonymous said...

Stop HARD WORKING)))
Only for man useful links )))

FOR FORCE buy viagra FOR REST casino
and for your girlfriend )))) fresh flower


i think its will be usefull ))))))

I found a lot of interesting information for me ))) here )))) and i start prepare to 8 march )))))

Anonymous said...

I start to women day prepear

I start to women day prepare……
I buy flower, viagra and xanax .....))))
But I have problem. I haven't women….
Help me please.

Anonymous said...

Best flower for you girlfriend
BEST FLOWER

soma or here phentermine

Post a Comment