Tuesday, May 16, 2006

Hivi Ipo Hii Peke Yake?

Kila kutokeapo dharura ya kuwataka viongozi kufika haraka katika baadhi ya maeneo, mfano majuzi wakati Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein anakagua mafuriko mkoani Kilimanjaro, helkopta hii ya polisi ndiyo hutumika. Najiuliza hivi hakuna nyingine? na je ikitokea nayo ina shughuli nyingine mfano ya kufuatilia majambazi hali itakuwaje? (-RSM-)

10 comments:

Anonymous said...

Tatizo letu TZ hatuna kitu kinachoitwa "Emergency Strategies" nadhani ni kutokana na kukosa sana Elimu na ujuzi wa "Public Relations" maana hii kazi ya kuratibu majanga ni pamoja na kuweka mikakati ya vitendea kazi vyake.Kuwa na kahelkopta kamoja ama tuwili ni hatari sana,nadhani kwa vile sasa kuna Wizara? ya maafa na majanga basi watendaji wawe wabunifu,ikiwezekana wizara zote isipokuwa ya Nje ziwe na Helkopta tayari lolote linapotokea.Wangeamua hivi nadhani hakungekuwa na malalamiko kama ya kununua magari ya gharama kubwa kwa ajili ya Waheshimiwa amabayo hayafai katika majanga. Nilikwenda katika mazishi ya Dr.Omar Juma kule Pemba nikaona umuhimu wa kuwa na Helkopta nyingi kuliko magari.Hongera RSM kwa changamoto hili.

Anonymous said...

Naunga mkono kwamba TZ hatuna "Long-term emergence Strategies" tunachojua ni "Zima Moto Style" na hata katika hizo, utakuta watu wanakurupuka kwenda eneo la tukio bila vifaa vya maafa, mfano magari mengi ya zimamoto, huwa hayana maji na wala hayapo katika style ya "Stand-by".Kuwa na Helkopta moja ni RISK kubwa sana na haitakiwi katika nchi kama ya TZ ambayo majanga yanaweza kutokea kila sehemu.Hivyo basi napenda niongezee ushauri wa annoy wa hapo juu kwamba Vifaa vyote vinavyotakiwa katika majanga ziwepo ili kurahisisha pale tatizo linapotokea, iwe ni mafuriko, nzige, kipindupindu, jengo kuanguka, meli kuzama ama kuzimika, kivuko kuzima injini, yote haya yanahitaji zana achilia mbali helkopta kutakiwa kukimbiza majambazi ama kutumika kukimbiza majeruhi. wakati umefika kuwa mna Mikakati imara dhidi ya maafa ambayo itahusisha pia kuwa na vifaa vingi na vya kutosha.

Anonymous said...

Aisee, RSM umenikumbusha mambo mengi.Hapa Morogoro watoto wanaiita helkopta ya Mahita(IGP-wa zamani, maana akija MG nbasi utasikia makelele na vumbi lake hapa viwanja vya Golf ama Polisi makao makuu. Nashangaa kwanini alikuwa anmatumia helkopta hata akija likizo, mtanieleza kama ni ofisi ama mtu mwenyewe.
Kuhusu wazo msingi kwa kweli ni lazima serikali iangalie umuhimu wa kuwa na zana kama hizo za kutosha,hasa helkopta, fikiria yakitokea mafuriko huko Ifakara amabayo yatahitaji watu kuokolewa kwa haraka tutafanyaye? watu si watakufa kama kule milimani Pakstani wakati wa Mtetemeko wa Ardhi ama kule New Orlens ama madhara ya Tsunami yalivyokuwa. Nashauri sijui hili lipo chini ya Wizara gani kulipa kipaumbele.Tunahitaji helkopta walau kumi.

Anonymous said...

Simon wachangia wako wanafurahisha sana kwa hoja zao. Ni kweli mambo mengi hayaendi vizuri Tanzania, lakini sio kila kitu. Na kwa maoni yangu kila wilaya angalau ingekuwa na chopa.

Tanzania kama nchi, inafahamu umuhimu wa kujiandaa na majanga, kwa muda mfupi na mrefu. Mfano kulinda vyanzo vya maji, ila wachangiaji hawajui hilo.

Kuita watu wajinga ktk suala kama hili kumenifanya nijue nani hasa mjinga.


Iweje wamesahau janga la Katarina kwenye nchi tajiri kwenye sayari hii na vitendea kazi vyote walivyonavyo lakini nini kilichotokea wachangiaji wanajua...strategy, emergence?

Mzarau chake huiba...

HSM

John Mwaipopo said...

Hivi tunatofauti kubwa sana ya uchumi na Kenya. Wakati wakenya binafsi tu kama waziri Nyachie anaweza kukodisha chopper lake kwa Mbowe, serikali yetu nzima bado inayo moja hiyo ya Mahita.

Anonymous said...

Janga la katrina ama la Tsunami tuajua lilivyoshughulikiwa na mapungufu yake katika strategies na hasa uzembe katika kuzingatia "warnings".hapa Tanzania tungekuwa na emergence strategies basi wale ndugu zetu akiwemo girl friend wangu wasingekufa pale Ziwa Victoria katiak janga la MV Bukoba, maana si swala la dakika moja bali lilidumu kwa muda ambao wangeokolewa.
Huu ni mfano mmoja tu na hat wizi wa Ubungo tungekuwa na realiable strategies helkopta ile ingewapata wezi wote ila tatizo lilelile, mipango ya zimamoto.Nakubali kuwa tuna safari ndefu ympaka tufikie huko,ukienda kila ofisi kuna vifaa vya zima moto lakini uliza wangapi wanajua kuvitumia.Angalia hiyo 999 kama ipo kweli active na wahusika wanaelewa maana ya kuitwa kwa kutumia 999, angalia kma Watz wangapi wanajua maana ya 999 kama ni emergency call line.Angali katika vyuo vikuu ikitokea moto kweny mabweni kuna simu ya kuita mara moja!hakika TZ bado kabisa ndio maana tuna kahelopta kamoja ka Mahita. Ikulu ilivyoungua uliona jinsi tulivyohangaika kuzima ule moto, karibu tuite watu kutoka South Africa kuja kuzima.
NI MTAZAMO

Anonymous said...

Ulinzi wa vyanzo vya maji! hakika hii ni strategy muhimu sana lakini hivyo ulinzi wake ni huo tu ama unahitaji vitu zaidi? sasa hivi kuna kitu kitwacho Global-environmental concern ambayo ipo chini ya Anti- Global warming Campaign. Athari za swala la Global warming ni kubwa sana kuliko ambavyo pengine sisi TZ tunafikiri,sasa hivi Barafu inayeyeka kutokana na joto, kumbe maji yataongezeka baadaye tikishayeyeuka yote yataanza polepole kupungua na kusababisha upungufu wa maji.Hapa TZ sawa tutalinda vyanzo vya maji kwa kivuli cha miti, vipi tunajiandaavipi na hilo joto litakalo kausha hivyo vivuli?je hili limo kweli katika strategies za nchi?kuna strategy gani juu ya barafu inayoyeyuka pale juu mlimani! tusijifanye kuwa tunamipango wakati pengine mipango yenyewe ni midogo sana, manafikiri kupungua maji kwa kidatu ama mtera kunatokana na kutotunza vyanzo vya maji?tembelea eneo hili la mto Ruaha utaona jinsi ambavyo swala hilo halipo, hili ni swala la Global-concern na mbaya zaidi hata katika malengo ya millenia sisi Africa ni Botswana tu inajitahidi walau.Sisi ni kupiga siasa tu hata katika mambo muhimu ya mazingira.

SIMON KITURURU said...

Kwa mtazamo wangu Bongo tuna historia ya kuandika, kuandaa na kuiongelea mipango ya muda Mrefu na mfupi, lakini hatuna historia wa utekelezaji wa mambo hayo.Utakutata tuna kuwa na mipango mingi yenye majina makubwa.Utakuta huu wa miaka 25 na huu miaka mitano lakini ukweli utekelezaji hauko kwenye syke zetu.Na hili moja ya jambo tunalobidi kubadili. Tusiende kwenye mambo makubwa, turudi pale kwa mwenye kioski.Kikiwa kipya rangi inang'ara na atakavyokuambia kuwa hiki ni kiboko na kitaendelea kuwa kiboko.Rudi baada ya mwaka utakuta kisha chakaa. Katika mipango yake ile rangi ilipopigwa wakati wa ujenzi ndio ilitoka tena.Twende kwenye hoteli.Zikifunguliwa babu kubwa njoo baada ya mwaka unaweza ukakuta hata vijiko vinauchache au vishakuwa kuukuu.Nausiende msalani kabla hujala unaweza kuondoa apitaiti. Kuna mifano mingi tu. Sababu kubwa ni ukosefu wa mipango ya muda mrefu hata kwa watu binafsi.Kumbuka Taifa na serikali ni watu.Hivyo kama Katika watu binafsi sifa hizi ni pungufu, serikali haiwezi kuwa vingine. Nauhakika hata hii helikopta labda hakuna hata mpango mzuri wa muda mrefu wa kuifanyia service. Utashangaa hata barabara zetu unakuta inatengenezwa leo ,tunaisifia kumbe hakuna mpango wa muda mrefu wa kuitunza .Baada ya miaka kazaa unaikuta ina mashimo tele.Kila mtu anamsukumia majukumu mwingine. DU hivi tunaye kweli Pailoti anayeweza kufukuza majambazi na Helikopta Bongo?

Anonymous said...

Really amazing! Useful information. All the best.
»

Anonymous said...

I say briefly: Best! Useful information. Good job guys.
»

Post a Comment