Saturday, May 06, 2006

Mtikila Aishinda Serikali

Yule Mchungaji Machachari, Christopher Mtikila, Mwenyekiti wa Taifa wa Democratic Party (DP) kwa mara nyingine ameshinda kesi nzito ya kikatiba ya Kutaka mgombe huru, asiyepitia katika chama chochote cha siasa, aruhusiwe kuwania ama ubunge au Urais wa Tanzania. nampongeza sana kwa uzalendo wake na sina cha kusema zaidi. Soma hukumu yake hapa. Itakumbukwa kuwa hii si mara yake ya kwanza kushinda kesi kama hiyo, kwani mwaka 1994, alishinda katika Mahakama Kuu Dodoma mbele ya Jaji Kahwa Lugakingira (+) lakini serikali ikakimbilia bungeni na kubadili Katiba ili kupinga hukumu hiyo. Sasa ameirejesha katika Mahakama ya Rufaa na kufanikiwa. Bravo Mtikila. Boniphace Makene aneye anamfagilia Mtikila kwa kazi hiyo.

5 comments:

boniphace said...

Hili ni tukio la pili linalonipa raha moyoni kufanywa katika siku chache zilizopita na mahakama za Tanzania ambazo niliwahi kuziweka katika kundi la mahakama za dola na sio zinazozingatia sheria. Kufutwa rushwa katika sheria za Tanzania na kisha suala hili la ugombea binafsi linatoa fursa la wasiotaka kujikomba kwa watu fulani sasa wajiandae kwa wananchi tu ili wakabidhiwe dola. Kwa Tanzania inawezekana kundi la wagombea binafsi linaweza kufanya vema kabisa katika nafasi za ubunge katika uchaguzi ujao kuliko nafasi za vyama vya siasa za upinzani. Na kisha kuna mgogoro mwingine ambao nitauzua baada ya siku chache, tega sikio tu ninaupika sasa!

John Mwaipopo said...

Haki ya mtu haipotei bali yaweza kucheleweshwa.

Panapo ukweli uwongo hujitenga.

Jeff Msangi said...

Taarifa muhimu sana hii hususani wakati huu tunapojaribu kuwa na demokrasia ya kweli.Nadhani wakati umefika wa sisi nao kuwa na mifumo yetu wenyewe na sio kuendelea kukumbatia mifumo iliyoachwa na wakoloni au kuiga kutoka kwa hao hao wakoloni.Yapo mengi ya kufanya..mahakama kama nguzo muhimu ya serikali inayo nafasi kubwa ya kubadilisha mambo..ikiachwa huru tu!

Anonymous said...

Mimi binafsi nimefurahishwa sana na juhudi za mwanaharakati Mtikila ambazo zimezaa matunda ya kisheria.Swali langu, JEURRI HII YA MAHAKAMA INATOKA WAPI?mbona hatukuiona hii mpaka wakati huu! kuna jambo hapa, nadhani ni hali ya kuleta mapinduzi ya kifikra amabayo yataleta maendeleo nchini.Kwa mtaji huu hata waliokimbia nchi hii watarudi maana haki ipo na inasikilizwa.

Anonymous said...

Your are Nice. And so is your site! Maybe you need some more pictures. Will return in the near future.
»

Post a Comment