Sunday, May 07, 2006

Kuna Haja wa Kuwa na Mbunge Huyu?

Mei 4, mwaka huu niliandika MAKALA hii katika gazeti la Mwananchi. Maudhui ya makala hii ni kutaka kujua kiwango cha elimu ambacho Mbunge wa Tanzania anatakiwa kuwa nacho badala ya mahitaji ya sasa ya Katiba, ya kumtaka awe anajua kuandika na kusoma kwa Kiingereza au kwa Kiswahili. Watu wengi wananiandikia wakitaka wabunge wawe na walau shahada moja. Wewe unasemaje?

4 comments:

Anonymous said...

Nafikiri lengo la katiba ya mwaka 1977 haikuwa mbaya, ilikuwa na lengo la kutoa nafasi kwa yeyote mwenye uwezo wa kuwa mbunge apewe nafasi hiyo.

Lakini ukiangalia dunia yetu sasa ndani ya karne ya 21 imesonga mbali mno na ile ya mwaka 1977 au hata 1990.

Mifano uliyoitoa (kwenye makala yako) inaonyesha dhahiri kuwa elimu ni muhimu sana, ili kuwakilisha watu wako hunabudi mwenyewe kuwa na upeo wa kutosha juu ya masuala mbalimbali ya kijamii, uchumi, sayansi n.k.

Ilikuwa makala fupi lakini imechokonoa suala muhimu sana kwa siha ya Taifa.

Anonymous said...

Sifa ya kuwa na Elimu ya juu na ya kutosha ni muhimu sana.Tatizo la watu wetu ni lile la kuangalia eti huyu ni mwenzetu, ama ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe ama anajua kuongea hii yote ni siasa na matokeo yake ni kuwa na Wabunge WANASIASA.Bunge la wanasiasa wasio na Elimu basi litaishia kushangilia hoja hata kama haina maslahi ya taifa, na hi hali ndiyo inalikumba Bunge letu.Nina uhakika Bunge lijalo 2010 ndiyo litakuwa Bunge hasa lillioenda Shule maana kwa sheria ya Wagombea Binafsi itatoa nafasi kwa MISOMI mingi kujiingiza katika kinyanganyiro na kufuta kabisa uanasiasa au umwenzetu.Hatuhuitaji sana kuwa na wabunge wengi wanasiasa, tutataka watekelezaji na walioenda shule.

boniphace said...

Hoja ya kiwango cha elimu ya wabunge kinabaki pale pale na hata wapiga kura wanajua hilo sasa. kAZI INABAKI KUWEPO KWA SDHJERIA ZILIZORUHUSU RUSHWA HALI INAYOWAFANYA WATU WASIO NA SIOFA KUINGIA KATIKA JUMBA HILO LA UWAKILISHI. Kuna kila sababu ya kupunguza uwakilishi wa watu wanaokwnda huko bila sifa za ujuzi wa mambo maana kutokana na kutofahamu mambo tumefika huku tulipo, sheria zinapitishwa bila watu kuzifahamu madhara yake mikataba inasainiwa bila kuchunguzwa na kisha ma IPTL mengi mengi yanajazana nchini ikiwa ni ujanja wa wachache. Anayedhani elimu haina maana akakae gizani kidogo kisha atatambua umuhimu wa kuweka kigezo cha elimu hasa kwa nchi maskini.

Anonymous said...

Interesting website with a lot of resources and detailed explanations.
»

Post a Comment