Tuesday, March 07, 2006

Waziri Akataa PhD Feki

Wakati mjadala wa Shahada feki za Udaktari wa Falsafa (Bogus PhD) unapamba moto (Jikumbushe Hapa), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Laurence Kego Masha, amelazimika kutumia zaidi ya sh 288,000 kuchapisha matangazo mawili katika gazeti la Mwananchi kupinga kuitwa Daktari (Dr/Dk.), wakati yeye si Daktari wa Binadamu wala hajasomea Udaktari wa Falsafa katika fani yoyote. Nimempongeza hapa kupitia gazeti hilo na kuwashauri wenzake wamuige.

11 comments:

mark msaki said...

Saaafi kaka Miruko! unawakilisha vizuri sana! tunakushukuru kuibua kimbembe! umetufanya hata wanablogu tufanye kazi kwa karibu na vijana wa kumekucha! inabidi ifikie kipindi mtu yeyote akitaka kuwa wa high profile basi na awe tayari kuwa mfano kwa wengine!

hadi huyu mkuu kuja kusafisha jina lake nadhani moto uliopo si mdogo!

je ni magazeti mangapi yameishaandika hii kitu? je makala yako ambayo ni safi na iko wazi kabisa imeenda kwa gazeti gani?

kama uliguzia ile habari ya ubalozi Italia! je kuna gazeti lengine limejimwaga leo huko nyumbani ukiacha DHW waliotupasulia sie wa huku?

kazi nzuri kaka Miruko! kanyaga twende!

John Mwaipopo said...

Kazi yako Miruko imetukuka na ikatukukika. Endelea hivyo hivyo.

Tumia uzoefu wako kuwachokonoa hao wengine. Najua itakuwa ngumu kuwataja majina katika makala zako lakini ujuzi na ubunifu wako utafanya jamii nzima iamke na ikishaamka itataka undani wa jambo hili. Hapo utakuwa umemaliza kazi.

Kwa msamiati mwingine, endeleza hoja huko gazetini kuchimbua hili lisilale.

Kila la heri.

mloyi said...

Nashangaa huyu jamaa alikuwa ni dk siku zote lakini leo ghafla anakataa yeye sio dk! Sijui unabii gani umemfikii mpaka kukataa huo udk. Umesikia PCB wamepewa meno makali zaidi sasa wameanza kujihofia baada ya mwenzao,dk. Mathayo David, kujulikana uongo wake! wako wengi wanaohitaji kuhojiwa hizo elimu wanazoongelea walizitoa wapi? mbona hazilingani na ufanisi wao wa kazi? au ndiyo zili za kupewa au toka vyuo visivyo na viwango?
Kazi imeanza.

ndesanjo said...

Chokonoa hasa Miruko. Ninafuraha kubwa kuona magazeti na hata blogu zinachimba mambo na kutupasha habari za mambo yaliyofichwafichwa.

Reginald S. Miruko said...

Baada ya article hii, Nimeletewa sms nyingi sana kuhusu suala hili. Wengi wamelaani kuwapo kwa vyeti vingi feki. Nimetajiwa hata baadhi ya majina naendelea kuyafuatilia, ingawa kuna ugumu wake kwani suala nyeti linalohitaji nguvu kubwa.

ndesanjo said...

Miruko, kwa kuwa wewe ni mwandishi na uko nyumbani, je unaweza kutafuta fomu za akina Matayo David tume ya uchaguzi? Na hata ya huyu aliyetoa tangazo gazetini. Kama amewahi kujiita mwenyewe dakta, hapo atakuwa na kibarua kigumu. Fomu za wagombea, ninavyofahamu, kisheria sio siri. Ni nyaraka za umma. Tafadhali. Uozo mkubwa huanza kwa kufichuliwa kwa mambo kama haya. Baadaye tutakuja kukutana na mengine ambayo hatutaamini.

Wako madakta wengi ambao wanajifanya ni madakta wa kitaaluma kumbe ni madakta kama dakta Remmy Ongala na maprofesa ambao ni maprofesa kama Maji Marefu.

mark msaki said...

Regnard, tafadhali usizidiwe, tuokoe hiki kizazi, kwa maana tukiwa na wakuu matapeli maana yake wataturudisha kule kule tusikotaka kwenda... nikiangalia hata mijadala ya EAC sasa hivi, inaonekana kabisa upande wetu (tanzania) umepwaya, sababu ya kuwa na wakuu wanaoaminiwa, wasiofaa kuaminiwa...tutaliwa tu kwa mwendo huu....

Miruko, kwa nini usiwe karibu na hawa jamaa wa www.kumekucha.com ? wao wamependekeza kufungua kesi...kuna haja ya kuunganisha nguvu hapa..

nyembo said...

kaka nimekubali,unatisha mno maana hii kazi yako si mkyezo, unajua wapo wengi hawa yakhe wenye kuvaa makoti na kuhitaji majina makubwa wakati wana elimu haba, inabidi zitumike njia kama hizi kuwaibua hawa!

frankj said...

safi sana,yeye anaujua umuhimu wa kuitwa dr na ndio maana ameamua kusahisha jina lake ili asimdhulumu baba yake cheo chake.yeye sio dokta sasa kwanini aitwe dokta.hao ndio tunaowataka bwana regnalid.

Ansbert Ngurumo said...

Kazi nzuri. Marsha amefanya hivyo wakati mwafaka, kwani wanamtandao wenzie wanamsaka kumchafua, na 'kumnyang'anya tonge mdomoni' eti kapewa wizara yenye ulaji wakati hakupambana kama wao kuhakikisha JK anapita!

Halafu umenikumbusha. Hivi udaktari wa Makamu wa Rais, Ali Mohammed Shein ni wa nini? Watu? Wanyama? Kubukua?

Reginald S. Miruko said...

Ngurumo, nimepokea ombi lako na kulifanyia kazi. Udaktari wa Makamu wa Rais, Dk. Ali MOhamed Shein uko hivi: Doctor of Philosophy (Ph.D) inClinical Biochemistry and Metabolic Medicine,
specializing in “Inborn Errors of Metabolism".

Kwa maelezo zaidi kuhusu CV yake soma hapa: www.kikweteshein.com/tanzania/pages/Vice-President

Post a Comment