Tuesday, March 21, 2006

Lowassa Hakosi Vituko

Waziri Mkuu, Edward Lowassa akipokea taarifa ya ujenzi wa shule ya msingi Manyara Ranchi, Monduli kutoka kwa Mkurugezi wa Programu ya ujenzi huo, Dk. James Kahurananga. alipokagua ujenzi huo, wakati wa ziara yake ya kutembelea jimbo lake la uchaguzi, Monduli, juzi. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Monduli, Onesmo Nangole na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Anthony Maley.

3 comments:

Anonymous said...

Miruko ukikutana naye mwambie vituko hivyo safi sasa apunguze makoti anapozunguka vijijini ili aweze wazi kufanana na raia wa huko.

John Mwaipopo said...

Miruko hiki kituko kimenichengua kwelikweli. Mbavu ziliuma almanusura nimuite dakitari. Nilipokuwa napasuka mbavu rafiki yangu wa Israel akaniuliza vipi wapasuka hivyo? Nikamueleza nae akakapasuka. Kapicha haka nimekatunza pale kwenye 'alibamu' yangu ili kasipotee haraka. Kazuri kwelikweli.

Jeff Msangi said...

Miruko,
Naona hapa Lowassa anawakumbusha watu kwamba "Mi mmasai bwana".Pengine alichosahau ni kwamba umasai au kuwa mtu wa watu hakuishii kwenye kuketi kwenye nyasi tu bali mambo mengine mengi tu.Lakini hata kwa hili anastahili pongezi na kutiwa moyo zaidi kwamba hata ukiwa nani na wapi utabakia kuwa wewe.

Post a Comment