Tuesday, March 28, 2006

Jengo Jipya la Bunge


Hili ndilo jengo jipya la bunge linalojengwa kwa ushirikiano kati ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Wamo NSSF, PPF, PSPF na LAPF. Gharama yake ni zaidi ya sh29.8bn. Lina uwezo wa kubeba wabunge 350 kwa pamoja, wageni maalum zaidi ya 100 na wananchi wasikilizaji 200. Linatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika wakati wa Bunge la bajeti Juni mwaka huu. Serikali italikodi hadi wajenzi warejeshe gharama zao na faida, kisha walikabidhi kwa serikali moja kwa moja. (Photo:RSM)

3 comments:

Martha Mtangoo said...

Kwa kweli Dogo jengo ni zuri lakini kwa mgeni ambaye ametoka matombo akija mjini hapa bila kuelezwa ni jengo gani hilo kwa hararakaharaka anaweza akadhani ni Msikiti au kanisa kuu la Roho mtakatifu la aNGLIKANA LA mjini hapa, me mwenyewe nililifananisha na msikiti wa Makka ambao mara nyingi nimekuwa nikiuona katika magazeti mbalimbali na Television sijui wenzamgu mnalionaje jengo hilo!!!!

msangimdogo said...

Kwakweli 'Kajengo' kametulia, nilibahatika kukatiza mahali hapo miezi kadhaa iliyopita wakati ujenzi unaendelea na kupata maelezo kiduchu kukahusu hako 'kajengo', hakika katawafaa sana wale jamaa wanaokesha sijui wakifanya nini halafu wakiwa ndani ya Bunge, husinzia kwa madai ya kutafakari hoja

MK said...

Kwa kweli jengo ni zuri sana tena sana ingawa gharama ni kubwa mno.

Sasa hizi gharama zinaweza kurudishwa kwa kufanya kazi kwa bidii kwa wote wananchi pamoja na wabunge wenyewe kutunga sheria za maana zitakazo leta maendeleo kwa Watanzania wote na taifa kwa ujumla.

Wasije wakazidi kusinzia Bungeni.

Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

Nashukuru,
©2006 MK

Post a Comment