Sunday, October 16, 2005

Sanamu la Nyerere Latua Dodoma

Zipo njia nyingi za kumkumbuka Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu 'Mtakatifu' JK Nyerere. Wikii hii nzima hotuba zake zilikuwa zimetanda katika anga za nchi. Makala zimeandikwa na matangazo kuchapishwa na magazeti, redio na televisheni. Msomi mmoja aliyepo Uingereza, Amani Millanga amenitimia makala hii juu ya Nyerere. Mjini Dodoma sanamu la Nyerere thamani ya sh 200 milioni limewasili kutoka Korea Kusini, litazinduliwa na Rais'mstaafu' Benjamin Mkapa, katika Uwanja mpya wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, katikati ya mji wa Makao Makuu iliyoshindikana. Kumbuka: Nyerere ndiye mwanzilishi wa wazo kongwe na kuhamishia Makao Makuu Dodoma, lakini nadhani wadau wenzake hawana nia hiyo katu.

9 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Indya Nkya said...

Ahsanye kwa hii makala. Ni murua sana.

Anonymous said...

Kuna swali naomba kuuliza tena naomba nipate majibu yaliyo na kina. Mwalimu kama alikuwa kiongozi mwenye sifa zote hizo nini kilichofanya asiandike (autobiography)au
asiandikiwe(biography)sharija ya maisha yake?

Nasubiri majibu yenu,
F MtiMkubwa Tungaraza.

Rama Msangi said...

swali la Tungaraza ni la msingi kabisa lakini naomba nami nimwambie au kumuuliza jambo hili: hivi kuna kanuni au umuhimu gani wa kila mtu mwenye sifa kama hizo au zaidi ya hizo kuwa na shajara ya maisha yake iwe kwa kuandikiwa au kwa kuandika mwenyewe?, Bado kwangu mimi huu ni moja ya tamaduni nyingi za kuiga (za kimagharibi), ambazo kwakuwa zipo tu basi watu wameona ni sehemu ya maisha na kuzipa umuhimu.

Kwanza angekuwa anamwandikia nani maana Watanaznia hawa hawa ndio wanaosemekana kuwa wavivu wa kusoma, sasa ingeandikwa ya nini basi?

Rama Msangi said...

@ RS Miruko:
Nilishuhudia sanamu zote za mzee wetu huyu zilizoleta kasheshe kule Mwanza na Tanga pia, je unaweza kunisaidia kujua hii ya sasa imekuja ikiwa imefanana na nani??

Reggy's said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Reggy's said...

Nawashukuru wote mliochangia mada hii na kuuliza maswali. Hoja ya Tungaraza mimi sina tatizo nayo, lakini nimetuma swali lake kwa mwandishi wa makala husika, UK, ili liweze kujibiwa. Tungaraza Ukiweza nitumie email adress yako, ili niweze kukupa majibu ya kina

Anonymous said...

Ndugu/Bwana Ramadhani, asante sana kwa hoja na swaki lako. Jibu langu ni kwamba historia ni kipengele muhimu sana katika maendeleo ya kihali na kimali kwa watu wa jamii yoyote ile. Kama hatutakuwa au hatutajenga tabia ya masijara (documentation) tuendelee kutegemea mapokeo ya historia toka neno kwa neno (fasihi simulizi) tutajikuta hatuna taswira za kujifananisha nazo (role models) na kila siku tunarudi kwenye tatizo tulilolitatua jana (solving today's problem with yesterday's solution and solving yesterday's problem with today's solution).

Pasingekuwa na maandiko ya watu mashuhuri leo hii tusingejua kama kina Mkwawa, Mirambo, Chaburuma, na wengineo walipigana kutetea uhuru wa himaya zao. Kwa mifano ya watu kama hao ambao walitumia nyute na mishale kupigana dhidi ya bunduki na mizinga tunapewa somo kwamba dhana ya kujitawala tulikuwa nayo, miundo ya utawala ilikuwapo, ari ya kujua kwamba ushindi wa vita siyo silaha kali tu bali ni kujitambua na kujithamini kunakupa nafasi ya kuheshimika miongoni mwa wanaulimwengu.
Tukichukulia mfano mwingine vitabu vitakatifu kama Biblia na Koran utakuta yaliyomo mule ni shajara za watu iwe ya Yesu, ya Muhamad, Ibrahimu, Abraham, Ayubu, Job, Daudi, David, Suleiman, Solomoni na wengineo zote zile ni shajara. Zisingalikuwepo leo tusingewajua na wengi wetu tusingekuwa hivi tulivyo hali kadhalika ulimwengu usingekuwa jinsi ulivyo.

Msemo wa samaki mmoja akioza wote wameoza siukubali katika suala hili. Wavivu wa kusoma tusiwafanye wenye nia ya kuandika waache kuandika kwa sababu siyo wote ni wavivuu wa kusoma. Kadhalika kwani hayo maandiko mengine aliyokuwa naandika alikuwa anamuandikia nani? Pamoja na uvivu wangu wa kusoma kitabu cha mwisho cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyere ambacho nilikisoma ni Uongozi wa Tanzania na Hatima Yake.

Jinginewe Ndugu/Bwana Ramadhani, utamaduni wa kimagharibi si wote mbaya hususani hili suala la masijara ni la muhimu iwe la kimagharibi, kimashariki, kikaskazini, au kikusini. Miye na wewe tumekutana humu kwenye maandiko kwa kutumia abjadi na nyenzo za Kimagharibi. Mwenyewe unaafiki raha tunayoisikia kwa kujua kusoma, kuandika, na kutumia hivi vifaa vya kimagharibi ambavyo vipo!

Ndugu/Bwana Ramadhani, nimepigiwa mbinje nishuke nikapate mlo na vijana wangu ambao wapo kwenye wanaumakinikia mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nakutakia kila la heri.

Watakabahu, ni miye maridhiya,
F MtiMkubwa Tungaraza.

Anonymous said...

Ndugu/Bwana Miruko,

Asante kwa kulipa uzito ombi langu na kulipeleka mbele zaidi.
Anuani yangu ni fidefide@yahoo.com

Masalaam,

F MtiMkubwa Tungaraza.

Post a Comment