Friday, September 16, 2005

Tanzania kuna nguvu ya media?

Vyombo vya habari duniani kote vina nguvu kubwa. Kama Tsunami. Kama Katrina na hata zaidi. Lakini kwa Tanzania, sidhani kama hali iko kama mahali pengine. Jumanne Sept 13, niliandika juu ya habari ya Askari Magereza kuwapiga waandishi wa habari na kuwajeruhi vibaya, kauli ya Waziri mwenye dhamana, Omari Ramadhan Mapuri na msimamo wa wamiliki wa vyombo vya habari kuwa "Waziri na Kamisha wa Magereza wajiuzulu". Hajajiuzulu hadi leo, na zaidi anasema kwamba tukio lenyewe ni dogo. Wenye vyombo vya habari ameweka msimamo mwingine, kuwa hawataandika habari zake wala za Magereza hadi Mapuri atoe tamko la kulaani na kukubali kuwajibika. Je, atafanya hivyo? Sidhani. Je vyombo vya habari vitaweza kususa habari zote za Mapuri? Vipi Gazeti la serikali, Daily News?, Vipi lile la Chama Tawala, Uhuru? Vipi Televisheni ya Taifa (TVT)? Naona ugumu. Watasuswa Makamanda wa polisi wote wa mikoa? zitasuswa habari za idara ya uenezi ya CCM? kila mtu ana maoni yake, tusemezane basi!

1 comment:

Indya Nkya said...

Nguvu ya Media Tanzania si ndogo. Suala la kujiuzulu ni kautamaduni ketu kabovu tuu, hata kama akishinikizwaje huenda asifikirie achilia mbali kujiuzulu kabisa. Dily News, TVT na Gazeti la chama si vyombo vya kuogopesha hata kidogo. Vina nguvu gani dhidi ya vyombo vingine vya habari vinavyopendwa na watanzania wengi? Hapa ni suala la waandishi walio wengi kuwa na msimamo. Kukataa kabisa kuandika habari zinazomhusu. Nina hakika nguvu ikiwekwa pamoja cha moto atakiona.

Post a Comment