Sunday, August 21, 2005

Wapya Katika Kuwani Ubunge Hawa Hapa

Nimerudi. Nasikitika sikukuageni. Nilikuwa napumzika kiduchu. Mara ya mwisho nilikuletea kwa ufupi mchakato wa kuwapata wagombea ubunge ndani ya Chama Tawala, CCM kuwa vijana wanawapa somo wazee. Sasa umekamilika, wapo wengi wapya, ama wapya majimboni au ni sura mpya kabisa. Nimekuletea ORODHA KAMILI, kwa Tanzania Bara nimeweza kuwawekea wapya alama '*' nadhani utaweza kuwatambua kwa urahisi. Kwa Zanzibar, nimeshindwa kwa kuhofia kukosea. Kila la Heri.-RSM-

1 comment:

Jeff Msangi said...

Ahsante sana kwa orodha ya wateule wa chama tawala.Nilikuwa naingojea kwa hamu.Nilichoweza kutambua haraka haraka ni kwamba kama asilimia 47% hivi ya wagombea bara ni wapya.Naona huo ndio mhemko wa nguvu mpya,ari mpya.Lakini pia nimeona kwamba kuna baadhi ya wagombea ambao sielewi wamerudi vipi.Lakini najua wapinzani hawatofanya makosa bali wataweka wagombea madhubuti.Natarajia mengi katika uchaguzi wa mwaka huu.Endelea kutumegea taarifa hizi muhimu.Ahsante sana.

Post a Comment