Wednesday, July 20, 2005

Kwa Nini Spika Awe na Chama cha Siasa?

Ukiangalia mgawanyo wa madaraka (Separation of Powers) kati ya mihimili mitatu ya dola, mahakama na bunge (Executive, Judicially and Parliament), kila mhimili unatakiwa kujitegemea, bila kuingiliana na mwingine. Leo nina swali, Je, ukisikia Jaji Mkuu kajiunga na chama fulani utamuelewaje? Na je, Spika wa Bunge kama huyu wa kwetu Tanzania, Pius Msekwa unamuelewaje anapokuwa mwana-CCM, tena Mumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu za chama chake? Mimi simuelewi. Wewe msomaji wa blogu unamuonaje? Anaweza kutenda haki kwa vyama vyote? naweza akakikandamiza chama cheke mbele ya vingine vya upinzania?

1 comment:

Rama Msangi said...

Mimi naamini kuwa umefika wakati wa kuwa na spika wa kuajiriwa kama katibu wa TFF, awekewe kanuni na misingi yake ya utendaji awe anafanya kazi kwa kuzingatia kanuni9 na mwongozo wake huo, zaidi ya hapo ni ngumu sana kuwa spika wa mfumo wetu wa sasa atatoa kura ya haki ikiwa atalazimika kuwa mtoa maamuzi kwakuwa kura yake itahitajika ikiwa ngoma inakuwa droo ndani ya Bunge. Kwanini walikomalia TFF washindwe wao???

Post a Comment