Friday, July 01, 2005

Daily Nation Yapinga Wakenya Kufukuzwa

Gazeti la Daily Nation la Kenya linalomiliki hisa nyingi katika Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, limepinga vikali hatua ya serikali kuwatimua na kuwapiga marufuku watumishi wake kufanya kazi Tanzania kwa kuingia nchini kinyume cha sheria bila vibali halali vya kazi. katika tahariri yake ya jana, Juni 29, The Daily Nation, liliweka wazi msimamo wake kuwa Wakenya hao warejeshwe kama njia ya kuimarisha uwekezaji na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment