Tuesday, June 28, 2005

Wakenya wa Mwananchi wafukuzwa nchini, wana dhambi gani?

VYOMBO vya habari Tanzania leo vimechapisha habari za kutimuliwa Wakenya sita waliokuwa wahariri wa magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) ya Mwananchi,The Citizen na Mwanaspoti. Sekeseke hilo lilianzia katika gazeti kongwe la Uhuru kuwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini, wanakwepa kodi kwa kulipiwa mishahara Kenya na kulipana kama posho badala ya mishahara.
Waliotumuliwa katika sekeseke hilo ni;
Mhariri Mtendaji wa MCL Mutuma Mathiu
Mhariri Uzalishaji Mbogo Murage
MhaririMaudhui (Content) Chaacha Mwita
Msanifu wa Gazeti Kizito Namulanda
Meneja Matangazo Waithera Munyoro, na
Mhasibu Mradi, Manjoi Kamau

No comments:

Post a Comment