Thursday, June 02, 2005

Bunge la Wasiwasi: Bunge linavunjwa, Wabunge nao 'wanavunjwa'

Dodoma hakukaliki.
Mguu mmoja ndani ya bunge mwingine jimboni kwa wapiga kura. Hayo ni mambo yanayotarajiwa kuanzia Jumanne ya Juni 7, hadi mwishoni mwa Julai bunge litakapovunjwa. Rais Ben Mkapa akipiga kipyenga pyeeeeeeee! kila mbunge atakuwa amevunjwa na kulazimika kukimbilia jimboni kutafuta uwezekano wa kurudi tena mwakani, ili kufaidi jengo Jipya la Bunge linalojengwa kwa sh bilioni 24. (Inadaiwa halipo Afrika). Yetu macho. NItakuwapa kila linalojiri.-RSM-

No comments:

Post a Comment