Friday, March 11, 2005

KAMATI KUU IKIGOMBEA YOTE NANI ATAMJADILI MWENZIE?

VIGOGO wa Chama Tawala, CCM, wameendelea kujitosa katika kinyang'anyiro cha urais, wengi wa vigogo hao ni wajumbe wa vikao vya HALMASHAURI KUU YA TAIFA na KAMATI KUU vya chama hicho.
Kiutaratibu, vikao hivyo vina nafasi ya pekee ya kupitisha majina ya wagombea urais, kabla ya kuyapeleka katika Mkutano Mkuu wa CCM kupigiwa kura ili kumpata mmoja atakayepambana na wapinzani.
Kama hivyo ndivyo, swali ni je, Kama Kamati Kuu karibu yote ikiwania uteuzi huo, nani atamjadili na kumpitisha mwenzie?

1 comment:

Anonymous said...

Hii imenichekesha hasa. Itabidi watuite wakereketwa tukawajadili.

Post a Comment