Wednesday, March 16, 2005

CCM ndio Mama Rushwa!

CCM ndio mama rushwa katika kumsaka rais. Ndio nasema hivyo na ninaamini hivyo!
Ni mama wa rushwa kutokana na mfumo wake Mfumo wa kuwapata wagombea wake. Mfano, gharama zake za kuchukua fomu ni sh 1,000,000. watanzania wangapi ambapo ni wasafi wanaweza kupata sh milioni moja (non refundable) bila kuteteleka?
Zaidi ya hilo, mgombea anatakiwa kuzunguka mikoa isiyopungua 10 mkutafuta wadhamini, walau 25 kila mkoa. wagombea wote wanaowania sasa wapo mikoani wakizunguka na wapambe wao kibao, wakikodi ndege kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, kwa gharama binafsi (si za chama). wanazipata wapi?
Mmoja wao, 'Mzee wa Ushindi' kama anavyotaka aitwe, alizungumza mikoa yote 26 ya Tanzania kwa siku tisa, na kweli kawa wa kwanza kurejesha fomu yake. Si mwingine ni Mzee John Cigwiyemisi Samwel Malechela (70). Wengine wanaojiita vijana, lakini wote wakiwa zaidi ya miaka 50 bado wanapishana mikoani na kufanyia vitimbi.
Mmopja wao, Dk. William Shija, amelazimika kuweka wazi kuwa yeye binafsi, kwa bajeti yake finyu, bila kuomba ufadhili wa mtu yeyote, anaweza tu kusafirisha wapamba wawili na kuwahudumia katika mikoa 15 tu. hatafika mikoa yote kama wenzake.
Msomaji wa blogu, inaonaje mawazo yangu, mimi niliyeamua kugombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo fomu ya urais ni sh 10,000 tu, ubunge sh 5,000 na udiwani sh 2,000. Zote fedha za madafu!. Fomu zenyewe zinapatikana hadi ngazi ya Kata hakuna haja ya kusafiri hadi Dodoma kuitafuta, wala kutafuta wadhamikni nchi nzima.
Watajiju.

No comments:

Post a Comment