Wednesday, February 23, 2005

Kipenga kimelia....On your marks, gets ready. Go....

Machi Mosi iko mlangoni. Ni tarehe muhimu kwa wapigania ulaji ndani ya Chama Twawala, CCM. Ndiyo siku iliyopangwa kuanza kuchukua fomu za kuingia jumba 'takatifu', ingawa sina uhakika kama wanaolikalia wote ni watakatifu kama lenyewe.
washiriki wa mbio hizo ni wengi, baadhi wamejitaja na wengine badi ingawa dalili zinaonyesha kwamba watajiunga katika mbio hizo za kupokezana vijiti.
Wakati wakimbiaji wanajitokeza kwa wingi, muda nao haujatulia. Unakwenda mbio. Huwezi kuamini, miaka 0 tayari imekwisha na Mzee Mkapa kamaliza muda wake wa kukaa Ikulu, kuzungukwa na walinzi na zaidi ya yote kukosa uhuru binafsi, japokuwa ana mamlaka makubwa, 'yanayokaribia' kuwa juu ya sheria. ka kweli, mzee huyu kaacha mambo mengi mazuri sebuleni na rekodi chache mbaya chumbani ikiwemo ya mauaji ya Wapemba wa Civic Unitred Front (CUF) ya Januari 26 na 27, 2001.hatujui atamwachia namni kazi hiyo ya juu kabisa nchini. Je, ni wale waliojitangaza, kina Sumaye, Simba au wanapotajwa kina Kikwete, Malecela, Mwandosya na....Yetu macho....

2 comments:

Anonymous said...

Kweli kipenda kimelia. Na yetu ni macho. Mkapa kaacha mazuri yepi???

Reginald S. Miruko said...

Kwa maoni yangu binafsi, siwezi kumbeza Mh. Mkapa. Hakika ameacha baadhi ya mambo mazuri tupende tusipende. Mosi, tungalie ukusanyaji wa kodi (hata kama haijamfikia mwananchi moja kwa moja), walau inatumika kujenga baadhi ya barabara pia,angalia maendeleo katika sekta ya elimu. Kwa urefu, nikipata wasaa nitayafafanua. Asante kwa kupitia blogu yangu mr/mrs anonymous

Post a Comment