"Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber."-Plato
Wednesday, May 13, 2009
Kubenea Akata Rufaa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halihalisi Publishers, wanaochapisha gazeti la Mwanahalisi, Saed Kubenea amesema anakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu iliyomtaka kumlipa fidia Rostam Aziz kwa kuandika habari za kashfa dhidi yake, habari kamili iko hapa. Inaelezwa kuwa yeye na wakili wake, Mabere Marando walichelewa kuwasilisha utetezi wao na vielelezo vyake mahakamani, kesi ikaamuliwa kwa kuangalia maelezo ya upande mmoja (ex-party), swali ninalojiuliza ni kwa nini Mwanasheria wake, mwenye uzoefu na uelewa, alichelewa kuwasilisha vielelezo na utetezi wa mteja wake. Kama nilivyoeleza kwenye story yangu iliyotanguliwa jana, magazeti kadhaa leo yameweka vichwa vya habari kuonyesha RA hausiki na Richmond
No comments:
Post a Comment