Tuesday, May 12, 2009

Du! Rostam Ashinda Libel Case

Habari za uhakika kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Rostam Aziz (pichani) ameshinda kesi ya kashfa (libel) dhidi ya gazeti la Mwanahalisi na Mkurugenzi wake, Saed Kubenea. Inaelezwa kuwa wadaiwa hawakuhudhuria mahakamani, hivyo, wakakumbana na hukumu ya upande mmoja (ex-party judgement). Wadaiwa wametakiwa kumlipa Rostam Sh3 bilioni, wamwombe radhi ukurasa wa kwanza kwa uzito ule ule, na walipe gharama za kesi. Kuna mtu ameandika maneno yafuatayo kwenye Jambo Forum:
"Mwanahalisi na Kubenea washindwa na Rostam
Hatimaye kwa nguvu za Mwenyezi Mungu alie hai mahakama kuu ya tanzania imetoa hukumu ya kesi kati ya kubenea na rostam aziz,mahakama imetoa hukumu hiyo tar 29 april,imemtaka kubenea amlipe rostam bilioni tatu pamoja na gharama za kesi kwa kumchafua hasa kuhusiana na richmond, thanx God. its me fisadi mtoto and my friend Dikteta"
Taarifa za ziada zinasema kuwa jioni hii kuna watu wanapitapita (hazikueleza wametumwa na nani) wakitaka habari zitakazochapishwa magazetini kesho zieleze kuwa: Rostam ameshinda kesi kwa sababu hakuna ushahidi wa kumhusisha na Richmond

No comments:

Post a Comment