"Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber."-Plato
Wednesday, May 13, 2009
Habari kubwa Leo
Yafuatayo yamechapishwa muda si mrefu kwenye mtandao wa Bidii
Magazeti yatia aibu kupotosha hukumu dhidi Mwanahalisi
Kuna habari kwamba baadhi ya wahahariri wa vyombo huru vya habari
wameomba Jukwaa la Wahariri litoe tamko kuhusu upotoshwaji wa
kimakusudi wa vichwa vya habari katika baadhi ya magazeti ya leo
kuhusu “Order” iliyotolewa na Mahakama Kuu chini ya Jaji Robert
Makaramba tarehe 30 April kuhusu kesi ya madai aliyoifungua Rostam
Aziz dhidi ya gazeti la Mwanahalisi.
Habari ambazo nimezipata kutoka baadhi ya wahariri wa magazeti
zinasema kuwa magazeti yanayomilikiwa na Rostam (Mtanzania na The
African) pamoja lile linalomikiwa na serikali (Habari Leo) yamepotosha
aliyoagiza jaji Makaramba kwa kusema kwamba mahakama imemsafisha
Rostam – kitu ambacho si kweli – Mahakama haikusema hivyo.
Wahariri wanadai kwamba alichofanya Jaji Makaramba ni ni kutoa amri tu
ya kuridhia madai ya Rostam katika shauri alililipeleka – bila kusikiliza upande wa Mwanahalisi – kwa sababu ya mawakili wa Mwanahalisi hawakuwapo Mahakamani. Kwa maana nyingine shauri halikusikilizwa kabisa, hivyo si kweli Rostam kasafishwa kuhusu madai ya umiliki wa kampuni ya Richmond.
Wahariri wanadai kuwa uandishi wa habari wa magazeti hayo yanakwenda
kinyume cha maadili ya uandishi na yametia aibu medani nzima ya
taaluma hiyo muhimu kwa umma.
Wahariri pia wamemuomba Jaji Makaramba kuyakemea magazeti hayo kwa
kuandika kile ambacho hakukisema katika “Order” yake.
By Yona Fares Maro
I.T. Specialist and Digital Security Consultant
No comments:
Post a Comment