Wednesday, April 06, 2011

Muswada wa Katiba wakera viongozi wa dini

HOFU NA MASHAKA YA WANANCHI KUHUSU
MUSWADA WA MAPENDEKEZO YA KUTUNGWA KWA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA YA NCHI YA MWAKA 2011


Kwa Waziri wa Katiba na Sheria

Mheshimiwa Waziri, Muswada wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi wa mwaka 2011 Namba 1 wa tarehe 11 Machi, 2011 umetangazwa katika siku chache zilizopita.

Baada ya kuusoma muswada huu tulishangazwa kuona kwamba mchakato wote unaanzia na kuishia kwa Rais na kwamba Chombo Kikuu cha kuratibu mchakato wote ni Tume itakayoteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama tawala.

Tunatambua kwamba kilio cha kutaka Katiba mpya kilitokana na utashi mwema na pia hasira njema ya jamii ya Watanzania wakitaka mabadiliko yaliyo na hekima na utu.

Tunahofia kwamba maudhui na mwelekeo wa muswada wa marekebisho ya Katiba unaopelekwa Bungeni havitakidhi mahitaji mazito ya watu na huenda ukachochea hasira ambayo imekwisha jidhihirisha katika jamii yetu.

Tunakuomba ulisimamie zoezi la marekebisho ya katiba kwa hekima sana ukiongoza tafakari jadidi na elimu angavu itakayowezesha zoezi lote kuwa la mazungumzo ya kitaifa kweli kweli huku amani, maelewano na makubaliano vikilindwa sana katika wakati mgumu huu.

Tafadhali lipatie taifa muda wa kufaa na chombo huru kinachoaminika kuongoza wananchi kufikia makubaliano yatakayojenga msingi imara wa taifa letu kwa wakati ujao.

Askofu Mkuu Paulo Ruzoka
MWENYEKITI
TUME YA HAKI NA AMANI (TEC)
5/4/2011

No comments:

Post a Comment