Ahadi za Kikwete:
- Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
- Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
- Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
- Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
- Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
- Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
- Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
- Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
- Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
- Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
- Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
- Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
- Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
- Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
- Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
- Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
- Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
- Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
- Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
- Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
- Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
- Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
- Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
- Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
- Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
- Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
- Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
- Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
- Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
- Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
- Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
- Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
- Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
- Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
- Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
- Kulinda haki za walemavu- Makete
- Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
- Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
- Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
- Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
- Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
- Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
- Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
- Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
- Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
- Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
- Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
- Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
- Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
- Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
- Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
- Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
- Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
- Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
- Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
- Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
- Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
- Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
- Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
- Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
- Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
- Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
- Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
- Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
- Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
- Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
- Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
Ahadi za Dk Slaa:
- Kujenga nchi isiyo na ufisadi
- Kurejesha maadili ya taifa, utumishi wa umma
- Kuanza mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100
- Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
- Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
- Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
- Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
- Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
- Kutoa huduma bora za afya bure
- Kutoa elimu bure chekechea hadi kidato cha Sita (elimu ya lazima)
- Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
- Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
- Kuwalipa wanaoidai DECI
- Kubana matuzi ya serikali
- Kupunguza ukubwa wa serikali (Mawaziri 15, manaibu watano)
Ahadi za Profesa Lipumba
- Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
- Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
- Kuunda serikali shirikishi
- Kusimamia rasilimali
- Kuimarisha miundombinu
- Kusimamia na kuboresha afya
- Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
- Kurudisha chakula cha bure mahospitalini
No comments:
Post a Comment