Thursday, December 10, 2009

Waanza Kulamba Asali

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad (wa tatu kulia) na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof Ibrahim Lipumba wakati wa gwaride la kuadhimisha miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu wa Rais, Dkt. Ali Mohamed Shein. Viongozi hao ambao hivi karibuni walimtambua rasmi Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar waliitwa na kukaa kwenye jukwaa rasmi la viongozi uwanjani hapo. (Picha na Emmanuel Kwitema)

No comments:

Post a Comment