Tuesday, August 18, 2009

Zombe huru, machozi yatawala

NDUGU wa wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro na dereva teksi wa jijini Dar es Salaam, waliouawa Januari 14 mwaka 2006 kwa tuhuma za ujambazi, jana walibubujikwa machozi baada ya Mahakama Kuu kuwaachia watuhumiwa wote wa mauaji hayo.
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Massati amemwachia huru aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Abdalla Zombe na askari wenzake nane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji hayo ya kukusudia, akieleza kuwa ushahidi haukujitosheleza kuwatia hatiani.
habari ndiyo hiyo. Mtiririko mzima wa kesi hiyo ulikuwa hivi. Watu wanaionaje kesi hiyo? Msomi wa sheria anaelezea: Sheria ndivyo ilivyo.

Maoni ya Msomi: Kilichotokea ni sawa na alichowahi kusema mwanafalsafa mmoja, Swift Jonathan (1667 - 1745) kwamba "Laws are like cobwebs, which may catch small flies but let wasps and hornets break through" --Damian Gabagambi kupitia Bidii

1 comment:

Anonymous said...

Poleni sana ndugu wafiwa, najua mtakuwa mmeumia sana kwa hukumu hii.najua mlitamani sana jana iwe siku ya kuwapoza moyo kutokana na vifo vya ndugu zenu lakini aikuwa hivyo. mungu awajalie moyo wa uvumilivu na matumaini pamoja na mapendo.Eleweni kuwa damu ya ndugu zenu akumwagika bure ipo siku ukweli utapatikana.

Binafsi nawalaumu sana waendesha mashitaka wa serikali eidha kwa kujua ama kwa kutokujua,kesi hii ilikuwa ifunguliwe kwa kutamkwa kuwa zombe na wenzie wamesababisha vifo vya watu hao. na wala si kuua. walijua kabisa kuwa katika kesi ya mauaji mara nyingi ushaidi unamwelemea yule aliyehusika kutoa roho ya mtu, kwa maana nyingine yule aliyeshika jembe ama panga ama bunduki na akaua kwa mkono wake. sasa sijui walipelekaje kesi ya namna hii wakati wakijua fika kuwa ushaidi wa mazingira unaweza kumuokoa zombe kwa kuwa siyealiyefyatua risasi na kuua.
Hata hivyo wanafamilia
Mnaweza kufungua kesi mpya kama ninyi mkimshitaki zombe na wenzie kwa kusababisha mauaji ya ndugu zenu. au mnaweza kukaa kimya na kumuachia mwenyezi mungu. kumbuka damu ya mtu aipotei bure.

Post a Comment