Tuesday, May 26, 2009

Wamepiga Kambi Busanda, Kazi Tumeiona


...Lengo la makala ya leo si kurudia yote niliyojadili na wasomaji wangu kwenye mada iliyopita, "Kampeni Busanda ni Jando ya Kisiasa" bali nitamtumia tu maoni ya mmoja wao. Huyu alijitambulisha kama John Simon wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Alihoji iweje mawaziri wa serikali ya awamu ya nne wapige kambi kwenye Jimbo la Busanda kukipigia debe chama kimojawapo, kwa muda wote wa kampeni na kutelekeza majukumu yao ya kuhudumia wananchi wote.

Hoja ya msomaji huyu ilinichoma. Niliifikiria mno hasa kwa kuwa mawaziri kwa fedha zangu za kodi.
Wanalipwa na wananchi wote ili wawatumikie wao. Hawalipwi mshahara na chama chochote cha siasa. Nimeamua kujadili hiyo hapa hapa leo kwa kuangalia mawaziri hao ambao hadi leo hii siku ya uchaguzi, bado wapo Busanda walipokuwa wanakipigania Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mara ya kwanza ilichapishwa Mwananchi Jumapili Mei 24, 2009. Kwa kina soma hapa

5 comments:

Anonymous said...

Kujadili jambo hili ni upuuzi mtupu!! nawashangaa waTanzania wenzangu kwa uwezo wao mdogo wa kuchanganua mambo.. viongozi kama wabunge, madiwani, mameya, mawaziri na Rais ni viongozi wa Kisiasa hawazuliwa na sheria yoyote kutumikia vyama vyao vya siasa.. tofauti na watu kama wakurugenzi na wengineo. acheni utoto!! unless mngesema itungwe sharia itakayotoa maelekeao kuhusu jambo hili. kama mwajifunza kuandika makala hapo sawa!! ndio maana Mkuchika, wabunge kama Zitto na Diallo hawakusita kwenda kusaudia vyama vyao huku wakijua wanatumia mafuta na mishahara ya serikali. Mmenielewa nyie watu!!!

Anonymous said...

We anony usiwe na hasira, kama wewe umeijadili hoja ya 'kipuuzi' kwa nini wengine tusiijadili? Miruko, usitishwe na huyu, endelea kutuwekea mijadala mizuri kama hii. Mimi sioni haja ya viongozi wa serikali kupiga kambi kufanya mambo a kisiasa. Kama anavyosema huyu anony kuna haja ya sheria kubadilisha ili kuondoa tatizo hili.

Anonymous said...

Haki ya mungu kuna watu hawana akili! Wewe umeandikiwa mawaziri, unang'ang'ania wabunge. Zitto na Diallo ni wabunge hawana ofisi ya Umma.
Unatukana watu kwa kujiona una akili za kukremu shuleni na kushindwa kupambanua mambo kutokana na kusoma shule kuwaza kuajiliwa.Jifunze kusoma vitabu uone wenye akili wanavyoandika (Anony wa juu).
Ndio maana unaona kila mtanzania hawezi kuchanganua mambo. Utakuwa fukara wa akili kwa kuona labda wazungu ama wahindi ndio wenye akili. Miruko uwe unaachana na hawa wenye akili fisadi. Ndio wanaoshika popote tunawaita mafisadi Pweza!!!
Unaweza kuwa katika managermenti level lakini bado ukawa nakili za kitarishi. Badilika Wakati ni Huu!

Anonymous said...

Wazo limetulia na kama hawa viongozi huwa wanapata muda wa kusoma magazeti tena makala kama hizi basi watakuwa wamelipata somo, ila nina wasiwasi kama siyo kufungua ukurasa wa mbele na wa nyuma(michezo) wamemaliza kusoma gazeti. Kwa upande wa internet nadhani wenye email wanaweza kuwa wachache pia.
Anony wa kwanza ni kuwa suala hapa ni mawaziri( wenye ofisi za umma na mishahara ya kodi zetu) siyo wabunge japokuwa nao kwa namna moja au nyingine tutawahusisha.
Kwa jinsi nilivyoziangalia hizi kampeni huyu mama angekuwa ni yeye pekee na wasaidizi wa chama ndani ya Busanda na Mwanza pekee wala asingeshinda mpaka kina Malecela,Ngeleja,Masha,Mkuchika,Magufuli+Wabunge wote wa Mwanza.
Mkuu Miruko wewe endelea kutuwekea mijadala kama hii usikatishwe tamaa wengine hapa ndo kwetu.
Aksante
Richy

Reggy's said...

Mimi sioni sababu ya kutojadilia suala hili. Hata huyo anony wa kwanza hajanishawishi, kama anaona mimi najifunza kuandika makala sawa, ni mchango wake pia. Ndio uhuru wa habari.

Post a Comment