Thursday, May 07, 2009

Kina Zombe Leo Majumuisho

ACP Abdallah Zombe


PC Michael Sonza


ASP Ahmed Makelle


WP Jane AndrewCPL Emmanuel Mabula
SP Christopher Bageni
CPL Abeneth saro

Kama mambo yatakwenda sawa, leo ndiyo siku ya kupanga hukumu ya akina Abdallah Zombe, yule bosi wa polisi Dar es Salaam, ambaye pamoja na askari wenzake wanashtakiwa kwa kuwaua wafanyabiashara wanne wa madini mwaka 2006. Ninapoandika haya, mawakili wao bado wako mahakamani wanawasilisha majumuisho--kwa wale 'learned brothers' wa sheria wanasema 'summotions'--yaani kutoa hoja (facts) zilizomo kwenye ushahidi ili kumsaidia jaji kufikia maamuzi. Habari Yenyewe ndiyo Hii.


Waliouawa:


Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo, na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa Manzese Dar e Salaam Juma Ndugu


Watuhumiwa:

Abdallah Zombe, SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, WP 4593 PC Jane Andrew, CPL Emmanuel Mabula, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisaba.


No comments:

Post a Comment