Saturday, February 07, 2009

Taarifa za Kina kuhusu sakata la Dk Slaa


Gazeti la Mwananchi liliandika haya:

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika mtandao wa internet kifaa hicho ambacho hutumiwa na wataalam wa ukachero, kina uwezo mkubwa wa kunasa sauti kwa muda mrefu kulingana na aina ya kifaa hicho.

Muda wa kunasa sauti huweza kuanzia saa 18 hadi 300 huku kikitumia kiasi kidogo sana cha umeme au betri. Kina kalenda ambayo mtumiaji huweza kuiseti kwa jinsi anavyotaka.

Kwa mujibu wa mtandao wa kampuni ya Ts- Market ya Russia inayotengeneza vifaa vya kunasia sauti katika mfumo wa video na sauti, kifaa hicho kina uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira ya kila aina ikiwa ni pamoja na vumbi na joto kali.

Pamoja na hayo, mtumiaji anaweza kuweka neno la siri kuhakikisha hakuna mtu mwingine anayeweza kutumia ikiwa ni njia salama ya kuhakikisha alichorekodi kinabaki salama. Pia kina chaguzi mbalimbali za lugha ambazo zinaweza kutumika. SOMA MWENYEWE

No comments:

Post a Comment