Friday, February 06, 2009

Sheria Mpya

CCM wapiga kura za ndiyo, Wapinzani wasema Hapana


Muswada wa sheria ya vyama vya siasa umepitishwa na bunge muda mfupi uliopita. Sheria hiyo ikipata baraka za rais itaruhusu vyama kuungana miezi sita kabla ya uchaguzi, lakini haitaruhusu viongozi wa kisiasa, eg wabunge, masiwani na rais kuhama na madaraka yao.

Sheria hiyo pia inaruhusu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali kukagua 'balance sheet' za vyama vya siasa. Wapinzani wameupinga kwa sababu walitaka uruhusu viongozi wa kisiasa wahame na madaraka yao kama ilivyo Kenya

No comments:

Post a Comment