Friday, February 06, 2009

Kisa cha Dk Slaa

Maswali kuliko majibu...

Kwa maneno yake, Dk Slaa anasema hivi: "Juzi saa tano wakati nahudhuria vikao bungeni, niliarifiwa na mmoja wa marafiki zangu kwamba kwenye chumba ninamolala kuna kinasa sauti cha kikachero.
“Mimi sikushtuka sana, nikawa naendelea na vikao bungeni. Kama unavyojua jana jioni nilikuwa nahudhuria kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
"Baada ya kutoka kwenye kikao hicho saa 11:00 jioni anilienda kula chakula cha jioni na saa nne usiku nilirejea hotelini. Nilipokuwa napanda ngazi, nikakumbuka onyo nililopewa na msiri wangu kuhusu kinasa sauti kwenye chumba changu.

“Nilikuwa nimeambatana na watoto wangu wawili na nilipoingia chumbani niliwaeleza kuhusu suala hilo la Bugging (uchunguzi wa kikachero) naona hawakunielewa lakini kwa kuwa nilishasoma novel nyingi zinazohusiana na mambo hayo nilijua nini cha kufanya.
“Kwanza tulichunguza kwenye sehemu za umeme za kuchomeka charger za simu, hatukuona kitu. Tukajaribu kufunua makochi nako hatukuona kitu. Tuakaanza kuchunguza sehemu zote zenye matobo hadi bafuni sikuona kitu. Tulipofunua godoro ndipo tukashuhudia lidude hilo kwenye chaga za kitanda.”
Baada ya hapo anaongeza kuwa waliita polisi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas KashililahDk. Thomas Kashililah na waandishi wa habari...Kwa mujibu wa Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Dodoma (RCO), Salum Msangia (RCO), Salum Msangia uchunguzi unaendelea, utazaa nini? ni tukio la kweli, ni mchezo wa kisiasa? fuatilia hapa...

No comments:

Post a Comment