Friday, February 20, 2009

Kigogo UVCCM alamba manoti


MGOGORO mpya unafukuta ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapiduzi (UVCCM, baada ya Kaimu Katibu wake Mkuu, Isaack Francis, kuenguliwa kwenye madaraka kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali na matumizi mabaya ya madaraka.Baada ya kumtimua Isaack, nafasi ya Kaimu Katibu wa UVCCM, inashikiliwa na Ally Issa, ili kupisha uchunguzi huru dhidi ya tuhuma zinazomkabili.Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zimesema kuwa uamuzi wa kumwengua Katibu Mkuu huyo, umefikiwa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilichofanyika siku mbili kuanzia Jumanne chini ya Mwenyekiti wa umoja huo, Masauni Hamad Masauni katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam. Soma Zaidi hapa

No comments:

Post a Comment