Tuesday, February 10, 2009

Hamad Rashid Atoa Hoja Binafsi

HOJA BINAFSI YA KUTAKA KATIBA YA NCHI IFANYIWE
MABADILIKO KWENYE BAADHI YA VIPENGELE
(Yametolewa chini ya kanuni ya 54 ya Kanuni za Bunge)
========================================




Mheshimiwa Spika,
Baada ya utangulizo nilioutoa katika maelezo yanahusiana na hoja,




KWA KUWA, Bunge ndicho chombo kikuu cha
kinachowawakilisha wananchi,




NA KWA KUWA,
Bunge ndicho kiunganishi kati ya Serikali na Wananchi,





NA KWA KUWA, Katiba inaeleza bayana
kuwa Bunge litaishauri Serikali katika utendaji wake wa kazi,





NA KWA KUWA, Katiba iko wazi sana na
inampa madaraka makubwa, uwezo mkubwa Rais aliyepo madarakani,





NA KWA KUWA, Madaraka hayo yanaweza
kutumiwa vibaya na Rais huyo ama kwa kuunda wizara nyingi sana yasioiletea tija
nchi yetu.





KWA HIVYO BASI, Ninaliomba Bunge lako
Tukufu lipitishe Azimio la kuitaka Serikali kufanya Marekebisho ya Katiba,
pamoja na mambo mengine kuweka vipengere vitakavyopelekea kuwapo na idadi ya
wizara zitakazokuwa zinaundwa na Serikali kutajwa bayana Katika Katiba na idadi
ya Wizara hizo zisidi 15 na idadi ya Mawaziri na Manaibu wao wasiozidi 25.
Sambamba na hilo kuweka vipengele ambavyo vitalifanya baraza la Mawaziri nalo
kuthibitishwa na Bunge kama ambavyo inafanyika kwa Waziri Mkuu.





Hamad Rashid Mohamed
Kiongozi
wa Upinzani na Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Wawi.

1 comment:

Jiaojiaofei said...

hello,I am from china,Nice to meet you.let's exchage our blog,which has chinese news in it.I thick we can be good friends.

Post a Comment