Thursday, February 12, 2009

DC awacharaza walimu Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali amewacgaraza bakora
walimu wa shule za msingi Katerero na Kanazi mkoani Kagera kwa kuwa shule zao zimefanya vibaya katika mitihanmi ya taifa.

Isome hapa...


MKUU wa wilaya ya Bukoba Albert Mnali, amemwamuru askari polisi mmoja kuwapiga viboko walimu katika shule tatu za msingi zilizoko Wilaya ya Bukoba kwa sababu wilaya hiyo imekuwa ya mwisho katika matokeo ya darasa la saba.Tukio hilo lilitokea juzi wakati mkuu huyo wa wilaya Koplo wa polisi aliyeambatana naye kwa kuwalaza chini walimu hao na kumuamuru koplo huyo kuwadhibu viboko viwili makalioni na mikononi.


Walimu waliocharazwa viboko tisa wanatoka shule ya msingi Katerero, 11 wa shule ya msingi Kanazi ambao walichapwa viboko viwiwili kila mmoja na walimu 12 kutoka shule ya msingi Kansenene viboko vinne vinne kila mmoja.Akizungumza jana waandishi wa habari juu ya tukio hilo mkuu huyo wa Wilaya alisema alilazimika kuwatandika viboko walimu hao baada ya kugunda au kuwepo uzembe kazini, ikiwemo kuchelewa kufika kazini na kutofundisha kama mikataba yao ya ajira inavyosema.


Alisema uzembe huo umesababisha wilaya ya Bukoba kuwa ya mwisho kimkoa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuwa uamuzi huo utasaidia kuwakumbusha wajibu wao.


Nikweli nimewachapa, mara hii nimechapwa wakiwa wamefungiwa, wakati mwingine watapigwa hadharani,” alisema Mnali.

No comments:

Post a Comment