Wednesday, January 21, 2009

Turudi Kwenye Mambo Yetu


Vichekesho havina kikomo. Jamaa mmoja kanitumia ujumbe (SMS) ufuatao: "Kila TV ukifungua utaona Obama, obama, utasikia Bush, Bush, nyingine Gaza, Israel, Palestina. Vyombo vya habari vya hapa utasikia Kagoda, Epa, Richmond na UDSM; magazeti nayo yamo, hatukai tukapumua...Sasa turudi kwenye mambo yetu: Hivi chura ukimtazama, kakaa, kachuchumaa au kasimama? Naomba jibu haraka ili niulize swali jingine.

No comments:

Post a Comment