Friday, January 30, 2009

Moto wa Bunge


Yule mbunge asiyetabirika wa Jimbo la Kwela, Chrisant Mzindakaya leo ameibuka upya bungeni akiwa na hoja moto binafsi iliyomlowanisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga--kama si huruma ya 'Bunge' mama huyo alikuwa amemwaga unga hadharani, lakini maamuzi yake yamebatiliswa. Utapata zaidi hapa, baadaye.
Leon Bahati, Dodoma

BUNGE limemkemea Waziri wa Maliasili, Shamsa Mwangunga kwa kuonyesha dharau dhidi ya maazimio yake ya kumtaka kusitisha umiliki wa vitalu vya uwindaji wa kitalii mwishoni mwa mwaka huu na badala yake kuwaongezea muda wawindaji hadi mwaka 2012.

Uzembe uliofanywa na Mwangunga, iliibuliwa bungeni na Mbunge wa Kwela, Dk. Chrisant Mzindakaya (CCM) kupitia hoja yake binafsi aliyoiwasilisha jana na kuungwa mkono na wabunge wengi.


Mwangunga aliamriwa kusimamisha vibali vilivyotolewa na wizara yake kwa wawindaji badala ya kuisha mwaka 2012 vifikie ukomo 2010 ili kuanzia hapo maazimio ya bunge katika kanuni mpya za uwindaji, yaanza kutekelezwa.

Vile vile, alikemewa vikali kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuigonganisha mihimili miwiuli, Bunge na Serikali kwa maana kwamba, akiwa na madaraka ya kiserikali iliyowekwa madarakani na wananchi alipuuzia mbali maagizo ya bunge, ambalo ni mwakilishi wa wananchi katika kutunga sheria za nchi.
Katika utetezi wake, Mwangunga alisema kuwa aliona kuwa kusimamisha ghafla kwa shughuli za uwindaji, kungesababisha hasara kwa taifa na hata kuathiri biashara hiyo, hivyo akanona ipo haja ya kuwaongezea muda wafanyabiashara hayo ili baada ya hapo miongozo hiyo ianze kutumika.

Alidai kuwa utoaji wa vitalu hupaswa kufanywa miaka miwili kabla ya kuanza biashara, ili kutoa nafasi ya mmiliki kutafuta wawindaji hivyo utekelezaji wa maazimio ya bunge ungeweza kulisababishia taifa hasara.


Aliomba radhi akisema kuwa hakufanya hivyo kwa kulidharau bunge bali kwa utashi wake pamoja na ushauri wa wataalamu wake, aliona kuna umuhimu wa kuliokoa taifa katika kupoteza mapato kupitia sekta hii ya uwindaji wa kitalii.

No comments:

Post a Comment