Sunday, January 25, 2009

Mbuzi Akamatwa kwa Ujambazi Naigeria


Mbuzi mmoja nchini Nigeria alijikuta akifikishwa kituo cha polisi baada ya kushukiwa ni jambazi lenye silaha aliyetumia uchawi kujigeuza mbuzi katika jitihada za kutoroka baada ya kukamatwa akiiba gari. Sungusungu nchini Nigeria walimkamata mbuzi mmoja na kumfikisha polisi kwa madai kuwa mbuzi huyo ni jambazi lenye silaha ambaye alitumia uchawi kujigeuza mbuzi katika kujaribu kutoroka baada ya kukamatwa akiiba akijaribu kuiba gari aina ya Mazda 323. "Sungusungu walikuja kuripoti kuwa katika pitapita zao usiku wakilinda walikuta kundi la vijana waliokuwa wakijaribu kuiba gari" Tunde Mohamed msemaji wa polisi wa mji wa Kware nchini Nigeria alisema. "Walipojaribu kuwakamata majambazi hayo yenye silaha, majambazi hayo yalifanikiwa kukimbia huku mmoja wao akijigeuza mbuzi" msemaji huyo wa polisi alisema. Polisi hawakuthibitisha kama ni kweli jambazi huyo alijigeuza mbuzi ila walithibitisha kuwa mbuzi huyo aliswekwa jela katika kituo hicho cha polisi. Taarifa zinasema kuwa mbuzi huyo aliwekwa ndani hadi pale mmiliki wake alipoenda kwenye kituo hicho cha polisi kumtoa mbuzi huyo. Imani za kishirikina zimeenea katika miji mingi ya Nigeria. Mwishoni mwa mwaka jana baadhi ya watu nchini humo walikuwa wakilalamika kupotea kwa viungo vya siri baada ya kusalimiana na mwanaume waliyekuwa hawamfahamu aliyekuwa akitumia uchawi wake kupoteza viungo vya siri vya wanaume. Sungusungu nchini Nigeria wamekuwa wakitumika katika maeneo mengi ambayo polisi huwa hawafiki nyakati za usiku.

No comments:

Post a Comment