Thursday, December 06, 2007

Jakaya Kikwete Mhh!!!


JK alikuwa maarufu kupita kiasi na watz walikuwa na imani kubwa naye. Kura alipata za kishindo zaidi ya 80%. Alipopimwa kwa mara ya kwanza na Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) miezi mitatu baada ya kuingia madarakani alionekana anaaminika kwa 78% alipopimwa tena na Taasisi hiyo Oktoba mwaka 2006 wenye imani naye walipungua hadi 67%. Utafiti huo hakubishiwa na mtu yeyote. Sasa REDET wametoa ripoti mpya ya utafiti uliofanyika Oktoba 2007 na kubaini kuwa idadi ya Watz wenye imani na utendaji wa Rais JK (pichani kushoto) imeporomoka hadi 44% Habari hiyo iliandikwa hivi katika Mwananchi. Vile vile Tanzania Daima iliibuka nayo hivi. Taarifa hizo zimeshtua watu wengi na kila mtu alikuwa na namna ya kulizungumzia. Soma maoni yao na hapa kuna mengine.

No comments:

Post a Comment