Tuesday, November 20, 2007

Magazeti Pendwa Unayajua?


Yalipoanzishwa, wato wengi waliyaita Magazeti la Udaku. Yakaongezeka, yakawa mengi. Fungua Hapa utakuta baadhi yake. Lakini Mmiliki wa idadi kubwa ya magazeti ya aina hii, Eric Shigongo yeye aliyabatiza jina tofauti, Magazeti Pendwa. Si ajabu kumkuta baba analinunua kwa siri, mama naye anakuwa na la kwake, watoto nao kila mmoja ananunua lake...kila mtu na siri yake, huku mauzo yakiongezeka. Kwa kuwa ni magazeti yanayopendwa kwa namna tofauti, nimeona niwawekee hapa na kwenye Kidirisha changu cha "Magazeti ya Tanzania" ili kila mmoja aweze kujisomea kwa wakati wake.

No comments:

Post a Comment