Tuesday, November 20, 2007

Kimyaaaaaaa!


Lile vumbi la maghorofa pacha ya BoT linaaza kutua. Kumbe hata ile tume tuliyoelezwa kuwa inachunguza gharama za ujenzi wake, inayotoa taarifa wiki hii, haijagusa majengo haya yanayodaiwa kuwa na thamani kuliko majengo karibu yote duniani. Inaelezwa kuwa inachunguza tu fedha zilizoingizwa katika External Payment Arreas Account (EPA), inayodaiwa kutumika katika 'kufanikisha' ufisadi. Upo hapo?

No comments:

Post a Comment