Wednesday, November 21, 2007

Dar Ndo Tanzania, Wengine Mtajiju!

Asiyekubaliana na hili atajiju. "Dar ndo Tanzania".
Unaweza kukataa ukipenda, lakini ukweli unabaki pale pale. Ninazo sababu lukuki, lakini kutokana na muda na nafasi nitaeleza moja tu. Majuzi tu, saruji ilipopanda bei Jijini Dar es Salaam kutoka Sh11,000 hadi sh15,000, kelele zimesikika ila kona, serikali ikaingilia kati na wazalishaji wa saruji wakaanza kutoa taarifa za bei. Kwa waliosikia, walidhani siku hiyo labda ilikuwa ya kwanza kwa bidhaa hiyo kupanda bei.(Kama huyu anavyoeleza) Kumbe, maeneo mengi ambayo 'labda'si Tanzania hali hiyo ilikuwa ya muda mrefu. Mfano Kanda ya Ziwa, Mwanza kwa muda mrefu ilikuwa si chini ya Sh15,000 na kule kina 'nshomile' ndo usiseme, ilikuwa Sh 18,500 kwa saruji ya Tanga, Tembo na Sh 17,500 kwa ile ya Uganda tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini usingesikia. Sasa anayebisha nani, kwamba Dar ndio Tanzania? Ndio maana tunazidi kujazana Dar.

No comments:

Post a Comment