Monday, November 19, 2007

Jua Limezama...Chadema Kunawaka Moto

HABARI MCHANGANYIKO

Leo nimeamua kukupatia mchanyato wa taarifa. Picha inaonyesha jua linavyozama. Wakati linazama, nimepata habari kemkem. Kwanza, ndani Chama cha Domokrasia na Maendeleo (Chadema) kunawaka moto. Zipo hisia mbili, Mosi, kwamba viongozi wamegawanyika baadhi wakitaka Zitto Kabwe aiteme Tume ya Kikwete ya kupitia upya mikataba ya madini, jingine likisema aendelee. Yeye anasema 'Nitaendelea hadi mwisho, labda JK aniondoe'. Sababu yake ni kwamba suala la kupitia upya mikataba ya madini limo ndani ya sera za Chadema na yeye amepewa opportunity ya kuipitia mikataba hiyo kwa niaba ya Watanzania na chama chake.
Pia wakati jua linazama, limeelezwa kuwa wale wagonjwa waliokosewa katika upasuaji Muhimbili, mmoja amekutwa na makubwa: Yaani yule aliyetakiwa kupasuliwa mguu akapasuliwa kichwa, amepooza upande mmoja; Na yule aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa amefanyiwa upasuaji uliokusudiwa leo. Soma maoni ya Zitto hapa Mambo haya!

No comments:

Post a Comment