Wednesday, June 28, 2006

Uhamishoni

Hii ni kwa Taarifa tu:
Mtajwa hapo kushoto, Reginald Miruko (RSM) kuanzia Julai 1, 2006 hatakuwa akiandika kwenye magazeti tando akiwa Dodoma. Mwajiri wake amemuhamishia Dar es Salaam. Hivyo akipata wasaa, licha ya majukumu yake mapya na mazito, atakuwa akikuhabarisheni akiwa jijini Bongo. Asanteni sana.

12 comments:

Anonymous said...

Inasikitisha kusikia unahama Dodoma kwetu sisi wengine ilikuwa kama jicho letu hapo.

Hata hivyo kila la kheri kwenye nafasi yako mpya nina imani itafungua ukurasa mpya katika kazi yako, na usisahau kutuandikia yale yasiyo kwenye "main stream media".

Ninaimani utapata muda japo sio mara kwa kutupa ya hapo Dar na picha pia kwani zinasema zaidi kuliko maandishi.

Anonymous said...

RSM nakutakia kila lililo jema hapo DSM, karibu sana Morogoro utakapotaka kupumzika wakati wa weekend, nadhani ombi la picha za kijiji cha serikali hapo MWANGAZA utalitimiza kutoka Dar. Ubarikiwe,msalimu Mwana Uwanja wa Hoja -OMEGA

Mija Shija Sayi said...

Hongera kwa kuhamia makao makuu ya nchi.

Vempin Media Tanzania said...

hongera kaka kwa kurejea 'Tanzania' tunakusubiri kwa hamu kaka. Ubarikiwe na Mungu akujaalie upate vingi zaidi ya hicho kimoja.

Simon Kitururu said...

Mr Miruko , Je unabadilishana na J Kikwete nini?Unapohamia Dar yeye atahamia Dodoma au?:-)Tunasubiri mavitu,Wajina.

Anonymous said...

halloh bro. miruko hongera sana na hiyo ni hatua moja ya maendeleo na umuhim wako katika kampuni,nadhani utaendelea kutufahamisha mambo mbali mbali yanayoendelea katika jiji kupitia print media. ok bro.
ni mimi simba, shabani ( B.A.mass communication student, muslim university of morogoro)

Simon Kitururu said...

Du Kumbe kuna Chuo Kikuu Kingine Moro!

Anonymous said...

Simon, chuo hicho kimeshazinduliwa rasmi tangu mwaka wa jama kumbe tayari watu wanatwanga masomo.Kipo pale Msamvu barabara ya kwenda DODOMA katika majengo ya kilichokuwa chuo cha Tanesco, ni kizuri sana kimajengo!

Anonymous said...

Heshima yako Mkuu. RSM inaelekea unamkimbia Makamba. Jitetee.

Reggy's said...

kusema kweli, simkimbii Makamba, tena ndo nimekuja karibu naye. Kwa sasa Makamba yuko bungeni, lakini muda mrefu yuko, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM. Usidanganyike, Makao Makuu ya CCM yapo Dodoma kwa jina, sura, viongozi, wasemaji wako Dar. Mtaa wa Lumumba. Pia, Makamba ni mbunge wa JIMBO LA IKULU-Magogoni Dar es Salaam. alamsiki

Anonymous said...

Miruko, naona umehama "mji mkuu" ukahamia "mji mkuu." Tukusanyie wafuasi zaidi hapo Mzizima.

Ansbert Ngurumo said...

Naona utashindwa kutimiza ombi na pendekezo la Ndasanjo. Sababu ni wazi. Umekuja makao makuu ya kweli, yamekuficha. Hujazoea? Hebu jikakamue utoke mafichoni. Wanablogu wanakumisi.

Post a Comment