Tuesday, May 02, 2006

Uhuru wa Vyombo vya Habari Unakuhusu?

Leo Mei 3 ni siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari. Sherehe za siku ya leo zinafanyika katika mji wa Colombo, Sri Lanka ambapo karibu watu 150 watashiriki kuwakilisha taasisi za habari, mashirika yasiyokuwa yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs), vyuo vikuu na taasisi mbalimbali. Kaulimbiu ya siku hii ni Mahusiano kati ya Uhuru wa vyombo vya habari na kuondoa umasikini. (Maelezo zaidi juu uhuru wa habari yapo hapa)

Kwanini iwe leo Mei 3?
Mey 3 ilichaguliwa kuwa Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari kwa kuwa ni siku ambayo Mkataba wa Windhoek ulitiwa saini mwaka 1991. Mkataba huo ni tamko la wachapishaji, wahariri na waandishi wa habari wa Afrika juu ya kutunza na kuendeleza Uhuru wa vyombo vya habari duniani kote (Hapa kuna maelezo zaidi juu ya siku hii). Imetolewa na zawadi ya UNESCO ambayo imekwenda kwa mwandishi huyu aliyenusurika katika shambulio la bomu.


Uhuru wa Vyombo vya habari unawezekana?
Ninavyoamini mimi uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu sana kwa jamii, ili kila jamii iweze kupata taarifa za kuelimisha, kuburudisha na kufahamisha. Ingawa yapo mataifa yaliyojitahidi kutoa uhuru kwa vyombo vya habari, hakuna hata moja ambalo linaweza kuijigamba kuwa vyombo vyake vya habari ni huru kwa asilimia 100. Jambo la kushangaza ni kuwa waandishi wengi bado wanauawa kinyama kutokana na habari wanazoandika Soma Hapa, uone jinsi mwaka jana pelee walivyouawa waandishi 63 duniani. Na Hapa kuna orodha kamili ya waandishi waliowahi kuuawa katika mataifa mbalimbali, kama ilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).


Uhuru ukitumika vibaya, kunani?
Hata hivyo, licha ya umuhimu wake, uhuru wa vyombo ni hatari sana pale unapotumika vibaya, kwani mambo yanaweza kuharibika na yakatokea machafuko na mifarakano katika jamii, mfano mzuri ni mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994 (Jikumbnushe Hapa).

Nani hutoa uhuru wa Habari?
Ukiacha mkono wa serikali, ili vyombo vya habari viwe huru lazma wanaovitumikia wawe huru pia na kuwa huru ni pamoja na kulipwa maslahi mazuri, ambayo yatapunguza (si kuzuia) wahusika kuingia katika mitego mbalimbali kama vile rushwa, upendeleo nk. Lakini kwa sasa waandishi wengi, hasa wa vyombo nilivyovizoea hawako huru katika ngazi hii, Soma Hapa, utagundua jambo. lakini pia lazima watu wote wanaotumia vyombo vya habari watoe mchango wao, kwa kutoficha habari na kusaidia katika kufichua, ili vyombo hivyo viwe huru zaidi. Kwa Tanzania, Waziri wa Habari Mohamed Sif Khatib, amekaririwa na BBC akisema kuwa Tanzania imepiga hatua kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara kwa uhuru wa habari. Kisa, eti kuna televisheni zaidi tya 20, redio zaidi ya 30 na magazeti na majarida zaidi ya 600. Je uhuru wa hivi unatosha?


Mie siwezi kueleza kila jambo hapa kwa kuwa naamini hata wewe msomaji unayo mengi ya kuchangia hoja hii.

SIKU NJEMA

11 comments:

Martha Mtangoo said...

RSM nimeyapata yote uliyoaandika huku, Duh!!!!!!!!!!!! baado sana ndo kwanza watu wamelala na wanaota ukuhusu uhuru wa vyombo vya habari inatia uchungu sana sasa sijui nifanyaje !!!

John Mwaipopo said...

Miruko hili suala la uhuru la vyombo vya habari ama mapambio kama anavyoyaita ndesanjo (kwa kazi ya kufagilia hata yasiyostahiki) lina pande nyingi tata. Sio uwongo watawala hasa katika nchi duni wamekuwa wakiukandamiza uhuru wao ilmradi kuona masuala yao hasi na chanya yanafanikiwa. Lakini Pia nyie waandishi kuna nafasi mnachangia. Katika kupitapita kwenye blogu yako nimeikuta makala moja nafikiri uliiandika ama mwezi wa tano mwanzoni ama mwezi wa nne mwaka jana "Kumuomba msamaa ndugu mgombea kwa kushiriki kumchafua". Makala ile sio nyepesi kama baadhi wanavyoweza kudhani. Ilikuwa inatoa taswira ya uandishi uliopo kwa sasa - kutumika na watu wengine kwa manufaa binafsi. Sio chanzo cha waandishi kudharaulika huku? Sio kutoa nafasi kwa 'magangwe' kukandamiza uhuru huu?

Alamsik Binuur

Reggy's said...

Mwaipopo ulosema ni kweli, kwamba hata waandishi wa habari na wenzao wanaijua kushika kalamu wanadidimiza uhuru wa vyombo vya habari. Nakushukuru kwa kurejea katika maktaba yangu na kufukua makala yangu kuomba msamaha, kwa niaba yangu na waandishi wenzangu. Nimefurahi kwamba uliielewa vilivyo. Nami nimeirejea leo ili kujikumbusha nilichokisema Mei mwaka jana.

Anonymous said...

Jamani uhuru wa vyombo vya habari haupo tu katika hoja alizotoa mzee Mengi kwamba waandishi wawe wasomi katika fani na mambo kama hayo nadhani mlisoma .Mimi niwaulize nyinyi wana habari kama kweli sasa hivi vyombo vya habari hapa TZ vina-practice Press Freedom maana vipo bised mno vinaandika mema tu ya serikali mpya, yanaandika juhudi za kupambana na majambazi mbona sasa hakuna vinavyo-challenge?Mnataka kutwambia kuwa hakuna mabaya mpaka sasa mnayoyaona kama wanahabari?mnafikiri ziara za kushukuru wananchi hazigharimu pesa?mnafikiri kukaa IKULU na kutoa hotuba ya kushukuru haitoshi mpaka zifanyike ziara?mnafikiri ni utamaduni kwa First Lady kwenda mikoani kutoa shukurani? Blair katika kampeni mkewe alitumia pesa nyingi sana kutengenezea mywele na hili lilizungumzwa sana ingawa lilipata watetezi, sasa mbona nyinyi hata hamthubutu kufuatilia CCM ilitumia kiasi gani kwa mgombea wake na kiasi gani alitumia First Lady katika kampeni hizo.Nyinyi wenyewe ni MAADUI wa Press Freedom, sasa hivi TZ hakuna media, bisheni hili!

Anonymous said...

Naunga mkono hoja ya hapo juu, TZ hakuna Media kwa sasa maana zipo biased sana na one sided, hata magazeti tuliyokuwa tunayaona yapo balanced sasa hivi mmmh hakuna kitu, wanamakala maarufu kwasasa inaonekana hawana la kuandika ama wameziba midomo, kila siku mema mema mematu, acheni hii, uandishi wa jinsi hii baada ya miaka kumi mtakuwa mmeua taaluma yote kabisa.Mnaogopa na hapo ndipo Press Freedom inavyokufa mikononi mwenu.Hili halina ubishi ndugu yangu uliyeandika hapo juu.

Anonymous said...

Somo zuri sana hili na umefanya vyema kutupatia takwimu kadhaa. Kuna jambo moja: hivi ni jambo gani linafanya vyombo vya habari/uongo vinavyomilikiwa na watu binafsi na makampuni kuonekana kuwa ni huru lakini vile vya serikali sio huru?

Ni swali tu, nataka kutazama watu wanafikiria nini.

Reggy's said...

Ndesanjo, sitakiwa kumiliki swali lako, lakini nitatoa maoni yangu, na wengine wasaidie kulijibu.

Mosi, Kwa mtazamo wangu, vyombo vya serikali ni mali ya umma, yaani ya wananchi wote lakini vinaonekana kuwa ngao ya watu wachache waliopo madarakani (wanajifanya kama wao ndio wamiliki), vinawalinda dhidi ya lolote ili waonekane wanafanya mema tu. Dhana hii, hapa Tanzania, haina tofauti na vyombo vinavyomilikiwa na watu binafsi, navyo vinawalinda wamiliki wake dhidi ya jambo lolote linalowagusa, lakini sura hii haionekani kwa umma, kwa sababu wanaolindwa ni wachache au anaweza kuwa ni mtu mmoja tu. Kwa hiyo, mbele ya macho ya jamii, vyombo binafsi huonekana kama mtetezi wao zaidi ya ilivyo vile vya serikali vinavyotetea kundi la watu wachache.

Pili, Vile vile vyombo vya binafsi vinataka kwenda zaidi kibiashara, usipojitahidi kuwa 'impartia' ukawapata wasomaji, watazamaji/ wasikilizaji kile wanachotaka, huwezi kupata wateja na utaondolewa sokoni bila kutarajia, suala hili halivisumbui sana vyombo vya umma. Wataandika chochote usiponunua 'utajiju' kwani wanapata ruzuku ama ya moja kwa moja kutoka serikalini au kupitia matangazo yote ya serikali na taasisi zake.
-RSM-

Anonymous said...

jamani hivyo kweli TZ hakuna media? mimi naona huyo jamaa kweli anachoongea hakuna critics katika media zote kwa sasa.Inavyoonekana kana kwamba media zote zimeshafauru kupata kile walichotaka sasa hakuna la ziada, hayo aliyotoa kama changamoto hakika ni kweli kabisa ni mapunguifu makubwa sana katika Press Freedom, na ni kweli wauaji wa Press Freedom ni media zenyewe.Hamuoni points za huyo jamaa?Wapi Rai, wapi Tanzania Daima, wapi Mwananchi?kwasasa mpo sawa na UHURU, MZALENDO,IPPMEDIA, DAILY NEWS NA SUNDAY NEWS, nyote ni pro-government, kama vile upinzani unavyokufa nanyi mnaua kabisa ile critical media, nadhani manangojea uchaguzi tena eti?toeni changamoto achaneni na ushabiki achaneni na kulinda maslahi ya waajili wenu teteeni taaluma itawalipa sivyo?

Anonymous said...

Anony hapo umenena wazi kuwa media zote sasa ni za kufagilia serikali, lakini lazima tukubaliane kwamba media zipo Tanzania ingawa hazikidhi mahitaji. Biasness ni kubwa miongoni mwake. Mimi nadhani hata hizo sheria zilizopo zinawabana, wengi wamefikia hatua sasa wanaona waandike ili wapate fedha zao. Investigative journalism kwa Tanzania ni ngumu kama vile 'kwenda mbinguni' ndio maana unasikia kiloa siku zinaibuka kesi za kudai damage ya sh 1 bilioni moja hadi majuzi ikatokea ya mfano ya sh bn 100 na Manji vs Thisday na Kulikoni, na mashakama inatoa, kama ilivyompa Dk. Salim sh bn 1 kutoka The East Africa. hayo yote yanatishia uhuru wa habari na vyombo vinaamua kuwa kama uhuru ulilolitaja.

Anonymous said...

Ni kweli kabisa mazingira ya Tanzania hasa sheria hizi za Defamation ama Invasion of Privacy zinashikiwa bango mno mpaka sasa kila mtu hata kama ni ukweli atatafuta kila njia kupindisha ukweli huo ili ashtaki. Ili kukwepa jambo hili nadhani ni kuanzisha gazeti la kila baada ya majuma mawili na litakalo fuatilia kwa kina habari kabla ya kuziandika, nina maana Investigative Stories. Hapa tutakuwa tumekwepa lawama na kujitetea kwingi kwa WATANZANIA pale wanapokumbwa na kashfa, swala hili la kuandika ili kuuza nalo pia tuliangalie linauwa taaluma ingawa tunapata pesa maana ni kuripoti tu tunakozingatia, sas mnafikiri ikifika mwezi Julai stori za serikali zitauza kwa wananchi? labda hizo za Bungwe na kama kuna jipya vinginevyo Mfumo wa Bunge letu hautoi chanagamoto watu kupenda kusoma habari zake.

Anonymous said...

Hmm I love the idea behind this website, very unique.
»

Post a Comment