Tuesday, April 04, 2006

Mark Msaki Yuko Dodoma

Halikuwa jambo la kawaida. Leo majira ya saa 9.00 mchana, nimekutana ghafla na mwanablogu mashuhuri, Mark Msaki ('Kurunzi' au Mwale wa Fikra) anayeishi Afrika Kusini. Nilikuwa katika eneo tunakula KITIMOTO (ashakum si matusi,namaanisha nyama ya nguruwe) katika klabu ya Reli mjini Dodoma. Alinitambua mwenyewe kwa kunifananisha na picha yangu inayoonekana kwenye blogu yangu. Aliniuliza kama mimi ndiye Miruko, nami nikaafiki. Akajitambulisha. Nilifurahi sana kumuona mwanablogu anayeishi ughaibuni ghafla kwenye mji wetu wa Makao Makuu yaliyoshindikana. Atakuwa Dodoma kwa takriban mwezi mmoja. Leo hatukuwa na kamera, baadaye nitakuleteeni picha tukiwa pamoja-RSM-

13 comments:

boniphace said...

Kama nali vile, hii ndiyo tunataka Miruko safi sana. Sasa kazi moja Miruko na Msaki tunaomba mjadiliane kuhusu misingi ya jumuiya yetu na ikiwezekana mtupe kabisa nini mnadhani tufanye na kisha tutalinganisha na mazungumzo yetu huku, ng'ambo ya pili na kutoka na kitu makini ili kudumisha safari yetu isiingiliwe na mamluki. Jadilini vitendo vya kihujuma vinavyoingia katika Magazeti Tando yetu na kisha hakikisgeni walau watu wawili wanashawishiwa kufungua magazeti tando haya toka hapo Dodoma hasa waandishi waandamizi kutoka Dom, safi sana Miruko nakupa five.

John Mwaipopo said...

Msalimie sana. Sasa najua kwa nini hatujampata kwa tusiku tuwili, tutatu hivi.

Hii maneno ya kumention 'Kitimoto' hadharani unanitia wivu wewe. Kitimoto bwana ziko Bongo. Tena nako sehemu na sehemu. Mathalani ya Arusha sikuipenda. Ya Dodoma sijawahi kuionja.

Alamsik Binuur

Anonymous said...

Miruko, kumbe Msaki amekuwa kimya kutokana na kitimoto cha mji mkuu ulioshindikana. Nilishangaa kaishilia wapi.
Kisa cha kukutana kwenu kinavutia, kumbe watu picha za kwenye blogu wanazitama kama askari anayekariri uso wa mhalifu. Naomba picha hizo mtutumie. Mjadili aliyosema Makene. Na mtuletee wanablogu wengine. Msaki fungasha kitimoto umpelekee Nkya!

Martha Mtangoo said...

Duh! kaka acha ubinafsi hata mimi pia nahitaji kumuona ukweli fanya kweli kaka haya mambo ya kuhadithiana mimi siyataki kabisa, fanya kweli!!!!!!!!1

Jeff Msangi said...

Nimefurahi kujua huyu bwana yuko wapi.Nina uhakika kurunzi lake litafanya kazi ipasavyo hapo Dodoma.Nina mjomba wangu hapo Dodoma-Coca Cola.Nitawaunganisheni nayo mkanywe coca na hicho kiti moto...au kiti moto kwa coca hakiendi??

Reggy's said...

Jeff, Kitimoto kwa coca hakipandi kabisa. hapo ni mwendo wa maji ya mende. Martha, usijali, kwa vile uko karibu, tukikutana na Msaki nitakujulisha uje umuone. Vile vile tutajadili yale yote, yaliyopendekezwa na wasomaji waaminifu wa gazeti hili tando

FOSEWERD Initiatives said...

si utani kwa kweli maana nilikuwa ninakula kitu moto pale railways karibu kabisa na stendi ya mkoa dodoma ndipo nikamuona mheshimiwa miruko akiwa kati kati ya wapambe wawili wakidodondoka nje ya double cab kwa minyato na usoni ungewasoma basi sura zilikuwa zimeandikwa KITU MOTO NA KIJE HARAKA SANA....kwa haraka haraka nikamwambia mamsap (maana ndo ananizungusha viwanja vya kula nyama)kuwa kuna mwanaserekali wa blogu ameingia akaniuliza ndio kitu gani hicho? na makao yake yako wapi? nikamjibu weye tulia ushuhudie, makao yake ni kunako cyber city.....hakuamini mpaka nilipomtambulisha kwa bwana Miruko...

ni kweli nimeamua kula mapumziko kwa ajili ya pasaka...hapa mwishoni nilikuwa nimetingwa na kuweka mambo vizuri kabla sijaachia chemba....

mwanablogu mark ni dereva, ameondoka Pietermaritzburg jumanne saa 10 asubuhi na kutinga mbeya alhamisi saa moja jioni... alitoka mbeya saa 6 mchana na kutinga dom saa 2 usiku..martha kumbe upoooo?? lazima tuonane miruko asilete longo longo!!

cheers!

Mija Shija Sayi said...

Siamini macho yangu! Yaani Mark hata kuaga?

FOSEWERD Initiatives said...

Mija mie mwenzio mtu mzima nimekuja huku ili nikusabahi!!! unapatikanaje? mie ni 0743 801044...makene upooooo!!!!!!

Rashid Mkwinda said...

Hivi kwa nini vijana wengi hupenda kitimoto, sijui kwanini hivi majui kuwa kitimoto kina madhara kiafya,poleni enyi mywao oo sory mlao kitimoto, hebu basi tuwatafute wataalamu watueleze madhara ya kitimoto na afya za wanadamu, mi nadhani tuifanye iwe mada ya mwezi huu katika Blogu, sizungumzii imani yangu ya dini bali tuitafakari kwa afya zetu, ili ikibainika kuwa haina madhara tuanze kushambulia.

Reggy's said...

Kuwatafuta wataalam ni vizuri, lakini kwa nini watueleze tu madhara na si faida za Kitimoto? unasemaje hapo Mkwinda? Kwa maoni ya walaji ni kwamba Kitimoto ni kitamu sana.

Rashid Mkwinda said...

Barabara oooh sory si hii barabara ipitayo gari bali ni Barabbara nadhani umenipata katika nimeshadidia katika herufi b ili ilete mantiki, kuna haja ya wataalamu watueleze hasara na faida ya Kitimoto kwa Afya zetu, twatamani kuila ila jinsi inavyochinjwa.....sory jinsi inavyouawa huwezi kutamani kuila kwani inapigwa bonge shoka kichwani bila hata huruma halafu kinachomekwa kisu katika shingo yake ili damu itoke, mazingira yake ukifika katika sehemu ya kuulia kitimoto hutotamani kukila

Reggy's said...

Mimi kama Mlaji, kama sina interest nyingine ya pembeni sina haja ya kujua nguruwe anachinjwa vipi! Ninachotaka mie ni nyama yake na taste yake. Ndo maana, hata Nyati, aliyeuawa kwa risasi, siulizi mie nakula tu. (Kumbuka nyati huwezi kumsogelea kumchinja kabla hajafa).

Post a Comment