Saturday, April 01, 2006

Leo Siku ya Wajinga

Leo ni siku ya wajinga. Wengi hawaijui siku hii, lakini kwa Tanzania, baada ya vyombo vya habari kuongezeka na siku hii imeanza kujulikana. Hii Siku soma hapa,Fools' Day (siku ya wajinga) ujue ilitokana na nini na kwanini watu wengi wanaienzi. Ebu cheki na Hapa uone jinsi watu wanavyodanganyana siku kama ya leo. Soma na Hii ya NIPASHE, uone uongo zaidi. Magazeti ya Majira na Mwananchi yamegongana kwa uongo wao leo, kuwa Kikwete amebadili Baraza la Mawaziri, isipokuwa Waziri Mkuu, na wengine wametimuliwa. Majira limeongeza kuwa Uwanja Mpya wa Taifa unaojengwa Dar Salaam umebomoka. kaa chonjo ynaweza kudanganywa zaidi leo.

4 comments:

Mzee wa Sumo said...

Hey Man kumbe na wewe ulipatikana lakini hukuwa na akili y akutambua lead ya The Citizen ya ajali Victoria kuwa ilikuwa hoax pia? Toka lini Meli ikatoka Biharamuro kwenda Muleba?

Mzee wa Sumo said...

Nimeanzish abog yangu, Mzee wa Sumo uipitie basi!

Reginald S. Miruko said...

Mzee wa Sumo, kutokuandika The Citizen hapa haina maana kwamba nilipatikana. Mambo kadhaa yanaweza kuwa yalitokea, sikuandika kila gazeti lilindika nini, yawezekana sikulisoma, lakini pia, Meli/boti kutoka Biharamulo kwenda Muleba inawezekana. Ziwa Victoria linapakana na wilaya zote mbili, katika maeneo hayo kuna visiwa ambavyo wakazi wake hutumia aina hiyo ya usafiri.

MK said...

Samahani ingawa haya siyo maneno yanayo endana na kichwa cha habari lakini naomba nitoe tangazo langu kuhusu blog.

TANGAZO:

Baada ya uchunguzi wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog).

Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

Jawabu la hili swali unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa.

Kama ukipata tatizo au maswali zaidi naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru,
©2006 MK

Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

Post a Comment